Diamond na mpenzi wake Zari katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV.
STAA wa
Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka kuwa
tayari amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' na
anatarajia kupata mtoto wa kike mwaka huu.
Diamond
ameyaongea hayo hivi punde katika Exclusive One on One Interview ya
Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV kuelekea katika shoo ya
Zari All White Party itakayofanyika leo usiku katika Ukumbi wa Mlimani
City jijini Dar.
Katika mahojiano hayo ambayo Diamond ameambatana na mpenzi wake huyo, ameongeza kuwa anatarajia kuingia katika ndoa mwaka huu.
Kwa
upande wa Zari yeye amefunguka kuwa bado hajajua jina watakalompa mtoto
wao wa kike anayetarajiwa kuzaliwa mwaka huu ila watampatia jina zuri la
Kiislam na lenye mvuto.
No comments:
Post a Comment