Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, May 2, 2015

LIVERPOOL ITAIWEZA QPR, MAN UNITED KUJIULIZA KWA WEST BROM LEO

Ligi Kuu England itaendelea tena Jumamosi na Manchester United wana nafasi ya kupanda hadi Nafasi ya Pili ikiwa wataifunga West Bromwich Albion Nyumbani Old Trafford.
Hivi sasa Man United wako Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Arsenal na Man City na Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wanahitaji kushinda Mechi 1 tu kutwaa Ubingwa.

Ushindi kwa Man United utawaweka Nafasi ya Pili, pengine kwa muda tu, kwa sababu Man City wanacheza Jumapili na Arsenal Mechi yao ipo Jumatatu.
Mbali ya Vinara Chelsea, ambao wanaweza kuwa Mabingwa Jumapili wakiifunga Crystal Palace, Man United, City na Arsenal, zikifuatiwa kwa mbali na Liverpool, Tottenham na Southampton, zinapigania kumaliza kwenye 4 Bora ili kucheza Ulaya kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu huko The Hawthorns, WBA na Man United zilitoka 2-2.

Jumapili City wapo Ugenini Jijini London huko White Hart Lane kuivaa Tottenham ambayo iko Nafasi ya 6 wakiwa bado wana matumaini ya kuingia 4 Bora. 
Jumatatu, Arsenal pia watakuwa Ugenini kucheza na Hull City ambayo iko vitani kujiponya kushuka Daraja na Mechi yao ya mwisho, Jana Jumatano Usiku, walipiga Liverpool 1-0.
Van Persie Uwanjani leo  Jumamosi dhidi ya West Brom Albion.LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Mei 2

14:45 Leicester v Newcastle
17:00 Aston Villa v Everton
17:00 Liverpool v QPR
17:00 Sunderland v Southampton
17:00 Swansea v Stoke
17:00 West Ham v Burnley
19:30 Man United v West Brom
Jumapili Mei 3
1530 Chelsea v Crystal Palace
1800 Tottenham v Man City
Jumatatu Mei 4
2200 Hull v Arsenal

No comments:

Post a Comment