Rais wa Shrikisho
la Mpira wa Miguu nchini –TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kuibuka na ushindi wa mabao
4-2 dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (The She-polopolo).
Katika salam zake
Rais Malinzi amesema ushindi walioupata Twiga Stars katika mchezo huo wa awali,
umetokana na maandalizi mazuri waliyoyapata chini ya kocha mkuu Rogasian
Kaijage, benchi lake la ufundi na TFF.
Aidha Rais
amewataka Twiga Stars kutobweteka kwa ushindi huo wa awali walioupata, bali
wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa ajili ya mchezo wa marudiano ili waweze
kupata ushindi na kuipeperusha vuzuri bendera ya Taifa ya Tanzania.
Mchezo wa marduiano
unatarajiwa kufanyika kati ya April 10,11 na 12, 2015, huu jijini Dar es alaam
na mshindi wa jumla atafuzu moja kwa moja kwenye fainali za Afrika kwa Soka la
Wanawake (All Africa Games Women) zitakazofanyika Brazzavile Congo Septemba 3-18
mwaka huu.
Twiga Stars
inatarajiwa kuwasili saa 7 kamili usiku (jumanne) jijini Dar es salaam kwa
usafiri wa Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Zambia.
Kwa niaba ya familia
ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wote wanawapa
pongezi Twiga Stars kwa ushindi
walioupata wa awali na kuwatakia maandalizi mema ya mchezo wa marudaiano.
Mabao ya Twiga
Stars katika mchezo wa jana dhidi ya Zambia (The She-polopolo) yalifungwa na
Asha Rashid (2), Shelder Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
No comments:
Post a Comment