LEO JUMATANO Usiku Uwanjani Stamford
Bridge Jijini London, Chelsea watakuwa Wenyeji wa Paris St Germain
katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA
CHAMPIONS LIGI.
Kwenye Mechi ya kwanza huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France hapo Februari 17, Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea Bao muhimu la Ugenini walipotoka Sare 1-1 na PSG.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza na kushinda 2-0 Uwanjani Stamford Bridge huku Bao lao la pili likipachikwa mwishoni na Demba Ba katika Dakika ya 87.
Eden Hazard 

Wakati Chelsea inatarajia kumrudisha Kikosini Kiungo wao Nemanja Matic ambae hajacheza tangu atumikie Kifungo cha Mechi mbli alichopewa baada ya kufungiwa kutokana na Rafu mbaya kwenye Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley Mwezi uliopita, David Luiz wa PSG anatarajiwa kurudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge tangu aihame Chelsea mwanzoni mwa Msimu.
David
Luiz, Mchezaji wa Kimataifa wa Brazil, alipozongwa na Wanahabari
kuelezea kuhusu Meneja wake wa zamani hasa kuhusu Lebo ya Meneja huyo wa
Chelsea Jose Mourinho kupachikwa ni ‘Mtu Spesho’ alijibu: “Ni spesho
kwenu si kwangu!”

Kwenye Mechi ya kwanza huko Parc des Princes Jijini Paris Nchini France hapo Februari 17, Branislav Ivanovic aliifungia Chelsea Bao muhimu la Ugenini walipotoka Sare 1-1 na PSG.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza na kushinda 2-0 Uwanjani Stamford Bridge huku Bao lao la pili likipachikwa mwishoni na Demba Ba katika Dakika ya 87.
Wakati Chelsea inatarajia kumrudisha Kikosini Kiungo wao Nemanja Matic ambae hajacheza tangu atumikie Kifungo cha Mechi mbli alichopewa baada ya kufungiwa kutokana na Rafu mbaya kwenye Mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley Mwezi uliopita, David Luiz wa PSG anatarajiwa kurudi kwa mara ya kwanza Stamford Bridge tangu aihame Chelsea mwanzoni mwa Msimu.
No comments:
Post a Comment