Gerrard akubali yaishe kimataifa, auvua unahodha wa England baada ya mashindano sita makubwa |
Nyota
wa zamani wa England na Liverpool Jamie Carragher amempongeza Steven
Gerrard kwa uamuzi yake ya kujiuzulu soka la kimataifa uamuzi ambao
ameutoa hii leo.
Carragher,
ambaye
aliwahi kucheza na Gerrard katika timu ya Taifa na klabu ya Liverpool
anaamini kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 baada ya kuitumikia
nchi yake kwa miaka kadhaa kwasasa anajiandaa kutoa msaada kwa kikosi
cha Liverpool katika vilabu bingwa barani Ulaya.
Akikaririwa na Sky Sports News Carragher amesema
'kwa Liverpool Football Club, ni maamuzi makubwa, ninaamini mashabiki wa Liverpool watakuwa wamefurahia.
Gerrard ameamua na iwe mwisho sasa kufuatia kukamilisha michuano mikubwa sita akiwa na England
UJumbe wa Carragher kwa Gerrard
Gerrard ameiongoza England katika fainali mbili za kombe la dunia na michuano ya Ulaya mara moja.
Siku za furaha: Carragher (kushoto) na Gerrard wakifurahia taji la vilabu bingwa mwaka 2005 |
No comments:
Post a Comment