|
Uvamizi: Wavamizi wa Kipastina wakionekana kuwavamia wachezaji wa Maccabi Haifa. |
Mtandao
wa klabu ya Maccabi
Haifa umechapisha taarifa iliyotolewa na nahodha wa klabu hiyo Yossi
Benayoun akiandika maoni ya vurugu zilijitokeza katika mchezo wao wa
maandalizi ya msimu mpya wa 2014/15 walipokuwa wakicheza dhidi ya Lille
ya Ufaransa huko Austria Jana na kupelekea mchezo huo kuvunjika baada ya
watu wanaodhaniwa kuwa ni Palestina walioko uhamishoni kuvamia uwanja
na kuanza kuwachapa.
Benayoun amesema
'Tukiwa kama klabu ya soka tunalaani vitendo vyote vilivyojitokeza ima kwa maneno hata kwa kushikana.
'Yesterday
(Jumatano) kuelekea dakika za mwisho za mchezo huo tulivamiwa na wahuni
uwanjani kwasababu sisi ni tunatoka Israelis. Tulikuwa hatuna la
kufanya isipokuwa ni kujilinda.'
Mbaya sana: Wavamizi wakimkabili wachezaji wa Maccabi Haifa wakitaka mchezo huo umalizwe mapema.
Vurugu: Wapingaji na wachezaji wa Maccabi Haifa wakipambana baada ya mchezo kusimamishwa.
Hili ni tatizo: Wachezaji wa Maccabi Haifa wakionekana wakijitetea baada ya uvamizi.
Wakati
huo Lille ilikuwa mbele kwa bao 2-0, wavamizi hao ambao wana asili ya
Uturuki waliingia uwanjani na wakiwafuata wachezaji waMaccabi akiwemo
nahodha wao Benayoun, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea, Liverpool
na QPR.
Mchezaji mmoja alionekana akimdhibiti shabiki mmoja kabla ya kumrushia konde zito..
Kocha wa Maccabi
Aleksandar Stanojevic amekaririwa akisema alijikinga na konde la mvamizi wa kipalestina kabla ya mwamuzi hajamaliza mchezo huo.
Wakijipanga na mabango yao kabla ya kuingia uwanjani.Chanzo kinasema mabango yao yalikuwa na ujumbe wanataka Palestina Huru
Afisa usalama mmoja akipambana na mvamizi mmoja.
No comments:
Post a Comment