Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski hawatakuwepo katika mchezo wa kuanza msimu mpya 2014/15 |
Meneja
wa Arsenal Arsene Wenger ametanabaisha kuwa nyota wake walicheza
fainali ya kombe la dunia hawatakuwepo katika mchezo wa ufunguzi wa ligi
kuu ya England 'Premier League' dhidi ya Crystal Palace.
Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski wanastahili mapumziko marefu kufuatia mafanikio ya Ujerumani nchini Brazil.
Watatu
hao hawatarejea kikosini wakati huu wa maandalizi ya timu mpaka Agosti
11 ambapo itakuwa imesalia siku tano kuelekea mchezo wa kwanza dhidi ya
kikosi cha kocha Tony Pulis.
Arsene
Wenger akipiga picha na nyota wa New York Red Bulls ambaye pia ni
nahodha wa zamani wa Arsenal Thierry Henry (wa pili kushoto)
Wachezaji wa Arsenal wakiwa mazoezini uwanja wa New York Red Bulls kabla ya mchezo wao wa kesho wa kujipima nguvu hapo kesho
Arsene Wenger akiongea na shujaa wake wa zamani Thierry Henry ambaye sasa anachezea New York Red Bulls
Wenger
amekataa kuthibitisha kuwa amemuadabisha nyota wake Jack Wilshere
ambaye alipigwa picha akivuta sigara Las Vegas lakini amedokeza kuwa
shirikisho la soka duniani FIFA linapaswa kufikiria upya juu ya ratiba
ya michezo yake ya kobe la dunia ambayo imetoa ugumu kwa maandalizi ya
kikosi chake.
Abou Diaby anaonekana kurejea upya msimu ujao baada ya majeruhi ya msimu uliopita, pichani anaonekana akiwa mazoezini New York
Mvuta sigara aliyeshindikana Jack Wilshere akionekana kujifua mazoezini Red Bull Arena jana.
Thierry Henry ameungana na bosi wake zamani Arsene Wenger pembezoni mwa wachezaji wa Arsenal wakati wa mazoezi
No comments:
Post a Comment