Hatimaye ratiba ya mchezo wa ngumi kwa mashindano ya Jumuiya ya Madola imetolewa leo tarehe 24/07/14 baada ya zoezi la kupima uzito na afya lililofanyika kuanzia saa 2.00 hadi saa 4.00 Asubuhi kwa saa za Scotland, kwa mabondia na waamuzi wote wanaotegemea kushiriki mashindano hayo`1.
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa mashindanoo yataanza tarehe 25/07/14 na yatamalizika tarehe 02/08/14.katika ukumbi wa Secc (Hall 4A) na inaonyesha kuwa captain wa timu ya Tanzania Selemani kidunda ndiye atayeanza kupeperusha bendera ya taifa na hatiaye kufatiwa na mabondia wengine kama ifuatavyo:-
Tarehe 25/07/14 saa 1.45 Jioni (69) kg
Kehinde Ademuyiyiwa (Nigeria) v/s Selemani Kidunda (Tanzania)
Tarehe 26/07/14 saa 7.20 Mchana (60) kg
Jessie Lartey (Ghana) v/s Nasser Maffuru ( Tanzania)
Saa 1.00 Jioni (64) kg
Stevin Thanki (Malawi) v/s Fabian Gaudensi (Tanzania)
Tarehe 27/07/14 saa 12.45 Jioni( 52) kg
Bye v/s Ezra Paul ( Tanzania)
Saa 1.40 Jioni (8I)kg
Mohamed Hakimu (Tanzania) v/s Sumit Sangwan (India)
Tarehe 28/07/14 saa 7.25 Mchana) (56)kg
Bashiri Nasir (Uganda) v/s Emilian Patrick (Tanzania)
Saa 1.35 jioni (49) kg
Paddy Barnes( Northern Ireland) v/s Hamed Furahisha (Tanzania)
No comments:
Post a Comment