Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, June 16, 2014

KOMBE LA DUNIA 2014: LIONEL MESSI UWANJANI USIKU HUU!!! ARGENTINA v BOSNIA-HERZEGOVINA

Leo Messi anatinga Estadio Maracana Jijini Rio De Janeiro wakati Argentina itakapoanza kampeni zake kwa kucheza na Bosnia-Herzegovina katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi F.
Baada ya kudorora kwa Lionel Messi Miaka minne iliyopita kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini, Mwaka huu tena mimacho iko kwake kuona nini atafanya.
Lakini Lejendari wa Argentina, Diego Maradona, anamatumaini Staa huyo atawika hasa baada ya ‘kupumzika’ kwa kukosa Mechi nyingi Msimu huu uliokwisha Juzi kutokana na kukabiliwa na Majeruhi.
Maradona ameeleza: “Naona Messi atafanya vizuri. Nadhani ilikuwa vyema kwake kupumzika baada ya kucheza Miaka minne bila kukosa hata Mechi moja.”
Maradona aliongeza: “Ningependa kuongea nae hivi sasa na kumwambia achukulie vitu kiulaini na asiwasikilize Wajinga. Bahati mbaya wako wengi hao!”
Akiielezea Timu ya Argentina kwa ujumla, Maradona ameonyesha wasiwasi wake kuhusu Difensi yao ambao Usiku huu itapambana na Bosnia yenye Wachezaji wasio na mzaha kama vile Edin Dzeko wa Manchester City.

Hata hivyo Safu ya Mashambulizi ya Argentina inampa mchecheto hata Kocha wao Alejandro Sabella na asijue acheze Fomesheni yake anayoipenda ya 5-3-2 au ya Mashambulizi ya 4-3-3.

Lakini, Wachambuzi wa Argentina, waliofuatilia Mazoezi ya Timu hiyo Wiki hii wanahisi Sabella atampiga Benchi Gonzalo Higuain na kuimarisha Safu ya ulinzi na hivyo kutumia 5-3-2 huku mbele wakiwa Aguero na Lavezzi na nyuma yao Messi.

Nae Kocha wa Bosnia, Safet Susic, amesema hawana mpangu kumuwekea Messi Mlinzi maalum.

Ameeleza: “Si vyema kwetu kupoteza Mchezaji mmoja ili amlinde Messi. Hatujawahi kucheza Mechi tukiwa na Mchezaji wetu kazi yake moja tu kumlinda Mtu mmoja na hili halitaanza kwa Argentina!”

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa Bosnia-Herzegovina kucheza Kombe la Dunia kwani ni Nchi changa iliyokuwa huru Mwaka 1995 baada kusambaratika kwa Yugoslavia..
Pamoja na Timu hizi mbili, Timu nyingine Kundi F ni Iran na Nigeria ambazo zitakutana Kesho.

No comments:

Post a Comment