Kikosi cha Tanzanite na benchi la Ufundi baada ya kurejea nyumbani leo |
Hapa wanapanda basi kuelekea kambini Msimbazi Centre |
"Mama na Mwana" Mchezaji Sherda Bonifice anajua kuzifumania nyavu akiwa na mama yake. Kwenye michezo miwili ana mabao 6 |
Mzazi aka Kenedy Mwaisabula alikuwepo kuwalaki vijana |
Baadhi ya wazazi waliokuja kuwalaki binti zao |
TIMU ya
Taifa ya wanawake U-20 “Tanzanite” imewasili leo saa 9.00 alasiri kwa
ndege ya LAM toka
Msumbiji ikiwa na matumaini ya kuifunga Afrika Kusini kwenye mchezo wa raundi
ya pili ya mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Canada mwakani.
Tanzanite
iliyokwenda kucheza na wenzao wa Msumbiji na kufanikiwa kuwafunga mabao 5-1
hivyo kuwafanya kuaga mashindano hayo kwa mabao 15-1 baada ya mchezo wa awali
kuifunga mabao 10-0 nyumbani.
Akizungungumza
mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, kocha wa timu
hiyo, Rogasian Kaijage alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kiasi kwamba
alilazimika kuwaambia wachezaji wake wacheze mchezo rahisi kutokana na kuhofia
kuonyeshwa kadi.
“Nashukuru
tumefuzu lakini hata wakati tunaondoka tuliwaahidi tunakwenda kufanya kile
ambacho watanzania wanakipenda ila mchezo ulikuwa mgumu mpaka nikalazimika
kuwaambia wachezaji wacheze mchezo rahisi (easy game)”, alisema Kaijage.
Akizungumzia
maandalizi ya mchezo ujao Kaijage alisema kuwa hategemei kufanya mabadiliko
sana kwani timu yake ni nzuri na wachezaji wanajua wanatakiwa kufanya nini na
kwa wakati gani hivyo atahakikisha kuwa anawajenga wachezaji kwenye utimamu wa
mwili na akili pia.
Naye Afisa
Habari wa Shirikisho la Soka nchin, Boniface Wambura, ambaye pia anakaimu
nafasi ya Katibu Mkuu wa shirikisho hilo aliwapongeza wachezaji pamoja na
benchi la ufundi kwa hatua waliyofikia na kuwa ahidi kuwatafutia michezo ya
kirafiki ya kimataifa ili wajipime kwani wanapokwenda ni kugumu zaidi.
Mechi ya kwanza ya Tanzanite
na Afrika Kusini itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya
Desemba 6 na 8 mwaka
huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment