Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, November 24, 2013

RAGE APINGA AGIZO LA TFF LA KUITISHA MKUTANO WA WANACHAMA NDANI YA SIKU 14

MWENYEKITI wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage,amepinga agizo la Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF,ambalo limemtaka kuitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama kujadi malumbano liyopo ndani ya timu hiyo.

Rage alisema amesikitishwa sana na TFF,kutokana na maagizo hayo ya kumtaka aitishe mkutano wakati kwa mtazamo wake alifikiri watakemeavitendo hivyo vya kufanya mapinduzi ambavyo vimepitwa na waati
“Siwezi kuitisha mkutano kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kupokonywa na madaraka yangu tena mbaya zaidi napangiwa hadi ajenda ya kuzungumza na endapo TFF,watanilazimisha kufanya hivyo nitajiuzulu,’alisema Rage.

Rage alisema kwenye katiba ya Simba ibara ya 28 kifungu cha kwanza (a),(b),(c) na (d) inamtambua Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na Wajumbe saba siyo Kaimu Mwenyekiti ambaye hatambuliwi na Katiba hiyo wala ile ya TFF.

Rage alisema Katiba ya Simba ibara ya (22)inasema Makamu Mwenyekiti wa Simba anatambuliwa kihalali kwa kuchaguliwa kwa kupata kura 50 +1 na Mwenye Mamlaka ya kuitisha Kamati ya Utendaji ni Mwenyekiti na siyo mtu mwengine.

“Kwa mujibu wa vifungu hivyo Joseph Itang’are bado hajawa na uwezo wa kuitisha mkutano wa Kamati ya Utendaji kwa vile hatambuliwi na Katiba ya Simba,”alisema Rage.
Mwenyekiti huyo alisema kutokana na makosa yaliyofanywa na viongozi hao kwenye katiba ya TFF,Ibara ya 73 adhabu za viongozi hao ni kufungiwa kwa miaka 10 kutojihusisha na maswala ya soka kwenye klabu husika.

Katika mkutano huo Rage ameongelea mambo mengi ikiwemo tuhuma za kula pesa za usajili wa mchezaji Emmanuel Okwi pamoja na fedha za udhamini wa Televisheni za ZUKU TV.
Pia kiongozi huyo alitumia mamlaka yake kama Mwenyekiti wa klabu ya Simba kumtangaza Michael Richard Wambura kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji huku aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Rahma Al Kharoos akiteuliwa kuwa Mdhamini wa klabu hiyo na amefuta mkutano wa Tarehe moja

Mapema wiki iliyopita Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ilitangaza kumwengua Rage kwenye nafasi yake ya Uwenyekiti na nafasi yake kukaimiwa na Joseph Itang’are, na kuitaarifu TFF,ambayo nayo ilipinga mapindizu hayo na kumpa siku 14 kiongozi huyo kuitisha mkutano ili kumaliza malumbano yao.

No comments:

Post a Comment