CHAMA cha Soka Mkoa wa Tabora, (TAREFA) kimelitaka jeshi la
Polisi Makao Makuu na Mkoa wa Tabora kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kuisadia timu ya Polisi Tabora kupanda Ligi
Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa Tabora
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora, (TAREFA) Yusuph Kitumbo amesema
kuwa nguvu ya pamoja inahitajika ili kuhakikisha Polisi Tabora inapanda ligi
kuu kwani imecheza daraja la kwanza bila kupanda kwa kipindi kirefu.
“Polisi Tabora inahitajika nguvu ya pamoja toka Makao Makuu
ya Polisi, Mkoa na sisi chama cha soka ili kuisaidia timu ipande daraja kwani
ipo nafasi ya tatu ikiwa ina pointi 12 kwenye kundi C hivyo tukishikamana
pamoja timu itapanda kwani ina wachezaji
wazuri japo inakabiliwa na matatizo ya kiuchumi na vifaa”, alisema Kitumbo
Kitumbo alifika mbali na kusema wameamua kufikia maamuzi
hayo kwani Poli ndio wamiliki wa timu hiyo hivyo wanapaswa kujua ushirikiano ni
muhimu kuliko ilivyo sasa kwani wachezaji wanasafiri kwa kutumia ‘pick up’ kitu
ambacho si vema kwa mchezaji kusafiri kwa magari ya wazi.
“Mchezaji anapaswa alipwe mshahara kwa wakati, apewe vifaa
na akae mahali pazuri nikiwa na maana ya malazi na usafiri ili afanye kazi yake
vema akiwa uwanjani, hivyo nawapongeza wachezaji kwa uvumilivu hadi hatua
waliyofikia”, alisema Kitumbo
Polisi Tabora inafundishwa na Kocha Mwinyimad Tambaza ina
pointi 12 nyuma ya JKT Kanembwa yenye pointi 12 ila zikitofautiana kwa mabao ya
kufungwa na kufunga huku Stand United ikiongoza kundi C ikiwa na pointi 13.
No comments:
Post a Comment