Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, October 1, 2013

RICH RICHIE AACHIA FILAMU MBILI KWA MPIGO

MUIGIZAJI nyota ambaye pia ni mtayarishaji na muongozaji wa filamu, Single Mtambalike 'Richie' baada ya kutamba sana na filamu ya Uyoga aliyemshirikisha msanii Yvonne Cherryl 'Monalisa' sasa  yupo njia panda asijue ni filamu ipi kati ya mbili mpya alizozikamilisha kwa mkupuo aanze kuiingiza sokoni. 
Filamu hiyo alizofyatua mkali huyo aliyewahi kutamba na michezo ya runinga kupitia vituo vya televisheni vya CTN na ITV, ni 'Kitendawili' na 'Likizo Hii'.
Richie alisema hajui hadi sasa filamu ipi kati ya hizo aanze kuingiza sokoni kutokana na zote kuwa bomba kwa ujumbe wake na namna washiriki wake walivyozitendea haki.
"Kwa kweli nipo njia panda mpaka sasa sijui nianze na 'Kitendawili' au 'Likizo Hii' ambazo nimezikamilisha hivi karibuni na zote zimechezwa na wasanii nyota nchini," alisema Richie.
Aliwataja baadhi ya wasanii waliozishiriki filamu hizo ni pamoja na Mzee Majuto, Chuchu Hans, Maringo Saba, Baba Haji na wengine.

No comments:

Post a Comment