Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

NYOTA WATANO WALIOWAHI KUTAMBA LAKINI WAMESAHAULIKA




LONDON, England
NI jambo la kawaida kwa wachezaji kung’ara kipindi fulani na kujizolea sifa nyingi katika tasnia hiyo ya soka hadi wanastaafu.
Hata hivyo bahati hiyo imekuwa ikiwakuta wachezaji kutokana na baadhi yao kung’ara na kisha wakatoweka kwenye ramani hiyo ya soka.

Katika makala haya tunajaribu kuangalia wachezaji watano ambao waling’ara wakiwa kwenye Ligi Kuu ya England kabla ya kutoweka kwenye ulimwengu wa soka.
1. Alex Song
Baada ya kujiimarisha katika nafasi ya kiungo katika timu ya  Arsenal na huku akionekana kuelewana vizuri na Robin van Persie, raia huyo wa Cameroon  alijinadi jina lake na kuwa kiungo mkabaji mwenye kiwango cha hali ya juu katika timu hiyo ya Gunners.

Lakini baadaye zikawapo taarifa za kwamba anataka kuitema Arsenal na baadaye Song akajiunga na Barcelona kwa ada ya pauni milioni 17.

Hata hivyo tangu ajiunge na vinara hao wa soka wa Catalan, Song hajawahi kutakata na watu tayari wameshaanza kusahau mtu anayeitwa Song.

Inaelezwa kwamba, kwa sasa kuna uwezekano ukamuuliza mtu yeyote kama amewahi kusikia mtu anayeitwa Song, pengine ukaambulia jibu la Song ndiye mtu gani?
2. Ibrahim Afellay

Huyo ni mchezaji mwingine ambaye alikuwa tishio kabla ya kujiunga na Barcelona na kwa sasa amesahaulika.

Alijiunga na timu hiyo kwa ada ya dola milioni 3 na akafanikiwa kumaliza msimu mmoja akiwa na timu hiyo ya  La Liga, ambapo alifanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na Ligi Kuu.
Hata hivyo baadaye alitoweka kwenye medani ya soka na kutokana na majeraha yaliyomfanya kukaa kando ya kikosi hicho, hakuweza kukomaa na kazi kama alivyokuwa mwanzo.

Kutokana na hali hiyo, msimu huu timu hiyo imempeleka kwa mkopo katika timu ya Schalke, lakini nako mambo yanaonekana kumuaribikia baada ya kukumbwa na matatizo ya misuli ya nyama za paja ambayo yatamfanya kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili.
Inaelezwa kwamba, kwa sasa nyota huyo huwezi kumkumbuka endapo hautakuwa uwanjani.
3. Salomon Kalou
Nyota huyo wa zamani wa  Chelsea, alipangwa kwenye mechi mbili za Klabu Bingwa Ulaya, moja ikiwa ni ile ambayo timu hiyo ilifungwa na ya pili ambayo timu hiyo iliweza kutwaa ubingwa.

Licha ya kuwa kati ya wachezaji waliopiga mashuti ya penalti, pia ni kati ya walioifanya Chelsea  kushindwa.

Baada ya kuonekana kwa mara ya mwisho katika kikosi cha  Blues na kutwaa nacho ubingwa, baadaye aliruhusiwa  kwenda kujiunga na timu ya Lille ya nchini Ufaransa.

Hata hivyo tangu atimke, naye amekuwa miongoni mwa wachezaji waliosahaulika na itamlazimu alazimishe kurejea kwenye michuano ya Ligi Kuu ya England, endapo atataka kurudisha jina lake kwenye ramani ya soka.
4. Florent Malouda
Nyota huyo pia ni kati ya  wachezaji waliotoa mchango mkubwa Chelsea na timu ya Taifa ya Ufaransa.

Nyota huyo aliwahi kucheza fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Ujerumani,  jambo ambalo analiona kama tunu kwake katika kazi yake ya kusakata kandanda.

Hata hivyo katika kipindi cha mwisho Chelsea alishindwa kupangwa kwenye kikosi cha kwanza na badala yake akawa akitumika kama mchezaji wa akiba.

Kwa sasa Malouda anasakata kandanda katika timu ya  Trabzonspor ya nchini Uturuki na mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya Ufaransa  mwenye umri wa miaka 33, amekuwa kati ya wachezaji waliosahaulika.
 
5. Aleksandr Hleb
Katika hatua nyingine, unaweza kumuelezea nyota huyo kuwa alikuwa mahiri kwenye kikosi cha Arsenal na mchezaji bora kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Belarus, kabla ya kujiunga na Barcelona ambapo alitumia muda mwingi akisugua benchi baada ya kuanzishwa kikosi cha kwanza mechi tano tu.

Baada ya kuondoka Barcelona, alitumia muda mwingine wa miaka minne akichezea klabu sita tofauti, lakini akashindwa kutengeneza jina lake.

Kwa sasa nyota huyo anachezea timu ya FC Bate Borisov na amekuwa akipondwa na mashabiki wa Arsenal wakimueleza kuwa asingepaswa kuhama ili aweze kufanya makubwa.

Kutokana na hali hiyo, Hleb naye anatumbukizwa kwenye kapu la wachezaji waliowahi kutamba, lakini kwa sasa wamesahaulika.

No comments:

Post a Comment