Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

HENRI JOSEPH NA ISSA RASHID "BABA UBAYA" FITI 100%




WACHEZAJI wa kikosi cha kwanza cha Simba, Henry Joseph na Issa Rashind ‘Baba Ubaya’, wako fiti asilimia 90, baada ya kukaa benchi kwa majuma kadhaa kutokana na majeraha yaliyokuwa yanawasumbua na kukosa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.

Akizungumza jana baada mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam, Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema jukumu la kuwachezesha wachezaji hao katika mchezo wa Jumamosi liko mkononi mwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Abdallah Kibadeni.

“Wachezaji hao wamerejea uwanjani leo (jana), wamefanya mazoezi pamoja na wenzao, hivyo jukumu la kucheza katika mchezo wa Jumamosi liko mikononi mwa kocha Kibadeni,” alisema Gembe.

Gembe alisema wachezaji, Abdallah Seseme na Adam Miraji hali zao bado si nzuri na wataendelea kuwa nje kwa muda wa wiki nne na wanaendelea kuhudumiwa kwa ukaribu na kufanyishwa mazoezi mepesi.

No comments:

Post a Comment