Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU HAAAAAKUNAGA



LONDON, England

LIGI Kuu ya England kwa sasa ni kama imekomaa, ambapo kwa miaka kadhaa yamekuwa yakishuhudiwa mabao yenye kiwango cha hali ya juu kutoka kwa wachezaji ambao hawawezi kusahaulika.

Wakati msimu huu zikiwa zimeshafanyika mechi takribani saba, jambo la kujiuliza ni kwanini msimu huu ligi hiyo inaonekana kuwa kali kuliko miaka yote.

1.                  Matumizi ya fedha
Tangu miaka ya nyuma Ligi Kuu ya England haijawahi kuwa na matumizi makubwa ya fedha wakati wa usajili, lakini mwaka huu klabu za Uingereza msimu huu zimevunja rekodi kwa kutumia pauni milioni 630 katika dirisha la usajili.

Kiasi hicho cha fedha kimevunja rekodi ya pauni milioni 500, ambazo timu hizo zilizitumia wakati wa usajili wa wa mwaka 2008.

Fungu hilo la fedha linadaiwa linatokana na fedha ambazo klabu zote zililipokea msimu uliopita, baada ya viongozi wa ligi hiyo kuingia mikataba na vituo vya televisheni ili kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye michuano ya ligi hiyo.

2.                  Mbio za ubingwa

Inaelezwa kuwa kwa miaka mingi ya nyuma, haijawahi kutokea idadi kubwa ya timu zinazofukuzia ubingwa wa ligi hiyo na badala yake zilikuwa ni timu nne tu zilizokuwa zikijitokeza kufukuzia ubingwa huo.

Hata hivyo msimu huu imeshuhudiwa msururu mrefu wa timu zikiwania kutwaa taji hilo.
Katika mbio za sasa timu za  Chelsea, Spurs, Man United, Arsenal, Liverpool na Man City, tayari zimeshaanza kuonesha mchuano mkali huku  Arsenal ikiwa imekaa kileleni kwa pointi mbili zaidi dhidi ya wapinzani wao.

3.                  Vipaji vipya
Wakati zikiwa zimeshatumia fedha kupindukia, kipindi hiki pia ni cha klabu za Uingereza kuongeza vipaji vipya.

Baadhi ya mifano ya vipaji vilivyorudishwa msimu huu ni kama Juan Mata, Christian Benteke na Michu.

Hata hivyo msimu huu imeshuhudiwa vikitua vipaji vingine vipya vyenye wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile Christian Eriksen, Mesut Ozil, Wilfred Bony, Maarten Stekelenburg, Willian na Ricky Van Wolfswinkel.

Mbali na vipaji vya wageni, pia kuna nyota wachache raia wa  England kama vile Andros Townsend na Ross Barkley ambao wameshaanza kuonesha uwezo wake kwenye michuano ya Ligi Kuu.

4.                  Timu hazitabiriki
Suala la timu kutotabirika ni kati ya vitu vinavyoongeza chachu katika ligi hiyo msimu huu na matokeo yake yamekuwa yakiwashangaza wengi.

Miongoni mwa matokeo yaliyowashtua wengi, ni kipigo cha mabao 3-2 ilichokutana nacho Manchester City kutoka kwa Aston Villa.
Mbali na matokeo hayo pia ilishuhudiwa mabingwa watetezi, Manchester United wakichapwa mabao 2-1 na  West Brom huku ikishuhudiwa  Chelsea chini ya Jose  Mourinho ikilala kwa bao 1-0  dhidi ya Everton.

Pia Aston Villa imeshuhudiwa ikilamba pointi zote tatu kutoka kwa Arsenal na huku  Southampton ikiiduwaza Liverpool kwa kuichapa bao 1-0.
Matokeo hayo yanaifanya Ligi Kuu hiyo kuonekana kuwa ngumu kuliko mtu yeyote anavyoidhania.

5.                  Msaada

Huku ikiwa imesheheni matangazo ya bidhaa za biashara, michezo ya video, Ligi Kuu haijawahi kupata msaada mkubwa kwa ajili ya klabu zote kama ilivyo sasa.
Kwa sasa Ligi Kuu inapatikana kila pembe ya duniani, hivyo kila mtu anaweza kuangalia ligi hiyo bora duniani.

No comments:

Post a Comment