Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

MOURIHNO ASHIKWA NA KIGUGUMIZI KUTOMCHEZESHA KEVIN NA BENITEZ AMFAGILIA WENGER



BUCHAREST, Romania

KOCHA, Jose Mourinho  ameshikwa na kigugumizi kwenye mkutano na waandishi wa habari, baada ya kutupiwa swali kuhusu kutomchezesha nyota wake,   Kevin de Bruyne ambaye anadai kuwa anaona  amekuwa akichukuliwa  kama mtoto mdogo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, kocha huyo wa Chelsea alibwatuka usiku wa kuamkia jana katika mkutano  na waandishi wa habari wakati akizungumza kuhusu mechi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu ya Steaua Bucharest, baada ya kutwangwa swali hilo kuhusu nyota huyo raia wa Ubelgiji.

Kwa sasa, De Bruyne anafanya mazoezi na timu ya watoto wakati kikosi cha timu ya wakubwa kikiwa safarini nchini Romania na kuna taarifa zinazoeleza kwamba, yupo tayari kuondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo litakapofunguliwa mapema  Januari, baada ya kukwaruzana na Mourinho.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyopo karibu na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, nyota huyo kwa sasa haridhishwi na jinsi anavyochukuliwa na anajihisi kama anafanywa kama mtoto.
De Bruyne anakuwa mchezaji mpya kukwaruzana na Mourinho, ambaye msimu huu amekuwa akimsugulisha benchi, Juan Mata na alipohojiwa kuhusu mchezaji huyo juzi kocha huyo alibwatuka na kuondoka kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

“Kevin hayupo mahali hapa na ni uamuzi wangu na mtazamo wangu,” alisema kocha huyo huku akionekana kuchukizwa na swali hilo.
“Hii ni ajabu kwani hakuna hata mtu mmoja ambaye anauliza kuhusu Mata. Wiki tatu zilizopita, mlikuwa mkizungumza kuhusu Mata, lakini kwa sasa mmegeukia kuhusu Kevin,” aliongeza kocha huyo.

Alisema kuwa anawashangaa kuona wakizungumzia kuhusu mchezaji ambaye hachezi ama kuchaguliwa ndani ya timu na akasema kuwa huo ni uamuzi wake, kwani kwenye timu ana wachezaji 11 ambao wanaweza wakacheza na amekuwa akiwateua kwa kuangalia kile ambacho wanakifanya uwanjani na mazoezini.

Katika usajili wa majira haya ya joto, De Bruyne alikuwa anawindwa na timu za Bayer Leverkusen, Schalke na Borussia Dortmund lakini akawekewa ngumu na baba mzazi wa nyota huyo, Herwig De Bruyne alisema usiku wa kuamkia jana kuwa watalipatia ufumbuzi suala hilo wakati wa usajili wa dirisha dogo litakapofunguliwa mapema Januari mwakani.
@@@@@@@@@@@@@@@

Benitez amfagilia Wenger

LONDON, England

KOCHA Rafa Benitez amemmwagia sifa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger akisema kuwa ndiye kocha bora kuliko wote wanaofundisha kwenye michuano ya Ligi Kuu ya England.

Benitez alitoa kauli hiyo mapema jana, wakati timu yake ya Napoli ikijiandaa kuivaa klabu hiyo ya Emirates katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Katika mkutano na waandishi wa habari wa kuzungumzia mtanange huo uliopigwa usiku wa kuamkia leo, Benitez alimpotezea Kocha wa  Chelsea, Jose Mourinho akisema kuwa kocha mkuu huyo wa Arsenal ndiye kinara kwenye soka la Uingereza.

"Wenger ni kocha mkubwa, ni mtu mashuhuri na ni mmoja kati ya watu wanaolifahamu soka la Uingereza.
"Ana uzoefu mkubwa Ulaya kwani Arsenal mara zote imekuwa kati ya timu nne bora na amekuwa akifanya kazi kubwa na huku akisajili wachezaji wazuri. Kwa hatua hii kila kitu kwake kimekuwa kikienda sawa,” aliongeza kocha huyo.

No comments:

Post a Comment