Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

WAMILIKI MAN UNITED WAMKINGIA KIFUA MOYES



LONDON, England
WADAU wa soka Manchester United wamemkingia kifua kocha wao, David Moyes wakisema kuwa kuchelewa kumkabidhi timu hiyo ndicho chanzo cha kufanya vibaya mwanzo wa msimu huu.

Wadau hao ndani ya timu hiyo, walisema jana kuwa klabu hiyo ilipaswa kununua mkataba wa Moyes wakati akiwa bado yupo   Everton, ili kumuwezesha kufanya kazi ya kusajili wachezaji aliowahitaji badala ya kumkabidhi timu hiyo ya  Old Trafford, Julai mosi mwaka huu.

Kauli ya wadau hao imekuja wakati klabu hiyo ikijiandaa kumpa kila msaada ambao kocha huyo anauhitaji ili kuweza kutatua matatizo yake wakati wa usajili wa dirisha dogo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, wamiliki hao wa Man United, wanajiandaa kumsaidia  Moyes wakati wa usajili huo wa dirisha dogo litakapofunguliwa mapema Januari mwakani, ili kuhakikisha kocha huyo wa klabu hiyo ya Old Trafford anaondokana na kipindi kigumu alichopo katika msimu wake wa kwanza.

Vyanzo hivyo vinaeleza kuwa baada ya timu hiyo kutotumia fedha nyingi chini ya  Moyes, vigogo hao watafanya kufuru wakati wa usajili huo wa Januari kwa kununua wachezaji kama beki wa timu ya Everton,  Leighton Baines na kiungo wa timu ya Atletico Madrid, Ander Herrera ambao wanampasua kichwa Moyes.

Kipigo cha Jumamosi ilichoambulia ikiwa nyumbani dhidi ya timu ya West Brom, kimeifanya Manchester United  kuning’inia kwenye nafasi ya 12 ya msimamo wa ligi, huku ikiwa imeshachapwa mara tatu kwenye ligi hiyo na Moyes ameshakiri kuwa timu yake ina tatizo la ukosefu wa wachezaji nyota duniani.
 
Mbali na wamiliki hao, pia nyota wa zamani wa timu hiyo  Gary Naville amewatabiria mabaya nyota wa timu hiyo akisema kuwa watatupiwa virago kabla ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Moyes kufukuzwa.

Kauli ya nyota huyo imekuja baada ya kocha huyo, Moyes kuzomewa na mashabiki wakati wa mechi ambayo timu hiyo ilifungwa na timu ya West Brom na huku wakilalamika wakisema kuwa  kocha huyo anapuuza ushauri wa kocha wa zamani wa timu hiyo, Sir Alex Ferguson kukaa naye katika vyumba vya kubadilisha wachezaji.

Hata hivyo, Neville ambaye ni kaka yake na Phil Neville ambaye ni mmoja wa makocha wa timu hiyo alisema jana kuwa, Moyes hawezi kwenda kokote kwa sasa bali baadhi ya wachezaji watafukuzwa kabla ya kocha huyo kuondoka.

“Moyes atapewa muda wa miaka mitatu ama minne ili  kujenga timu na kujifunza mengi, itamchukua muda na atapewa muda kama ilivyofanya Arsenal kwa Wenger,” alisema nyota huyo wa zamani ambaye ni wa pili kuichezea timu ya Taifa ya England kwa muda mrefu.

“Tatizo hili naliweka kwa  wachezaji, kwani nawafahamu wote wanaweza kukufanya kuwa mwenda wazimu,” aliongeza nyota huyo huku akisisitiza kuwa wachezaji wengi watatimuliwa kabla ya Moyes  kuondoka.

“Niamini mimi wachezaji wote wataondoka kabla ya David Moyes kuondoka, kwa sababu atapewa muda,” alisema nyota huyo ambaye aliwahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara nane katika kipindi cha miaka 19 aliyokipiga Man Utd wakati akizungumzia mjadala kuhusu kama Moyes alikuwa mbadala kumrithi Sir Alex Ferguson.

No comments:

Post a Comment