Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

CANAVARO: TAMBWE HANITISHI




ZIMEBAKI siku 18 tu kabla ya kufanyika kwa mechi ya watani wa Jadi Simba na Yanga.
Lakini nahodha wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema kuwa hajaona jambo geni kwa mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe, kwani alishakutana na wachezaji wenye viwango vya kimataifa kama Samuel Eto’o na Didier Drogba.

Cannavaro ambaye ni beki wa timu hiyo na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' alisema jana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu yake kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola kuwa hamuhofii mchezaji huo kwani kwake anamuona ni mtu wa kawaida.

Alisema kuwa kwake Simba ni timu ya kawaida, kwani wameshakutana mara nyingi hivyo hana shaka nayo, kwani hata katika mchezo wao wa mwisho wa kufunga Ligi Kuu msimu uliopita, waliweza kuwafunga mabao 2-0.
"Kwa upande wangu huyo Tambwe simuhofii, kwani naamini kuwa ni mchezaji wa kawaida tu, hana kiwango cha kutisha na Simba ni timu kama nyingine, hivyo ushindi ni lazima."

Akizungumzia mechi yao ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar, Cannavaro alisema kuwa wanaendelea kijinoa kwa ajili ya mechi hiyo, lakini wanaimani kuwa watashinda kwa vile kocha amefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita.

No comments:

Post a Comment