Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 2, 2013

AMIS TAMBWE AUGUA GHAFLA AKIWA MAZOEZINI KINESI





MSHAMBULIAJI tegemeo wa Simba, Amis Tambwe jana aliugua ghafla wakati akifanya mazoezi na wachezaji wenzake kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam na kumfanya awe nje ya uwanja kwa ajili ya kupata matibabu kutoka kwa daktari wa timu hiyo, Yasin Gembe.

Mchezaji huyo alipatwa na ugonjwa wa tumbo uliomkumba ghafla jambo lililofanya baadhi ya wachezaji wenzake pamoja na daktari kuacha mazoezi na kumhudumia mchezaji huyo raia wa Burundi.

Akizungumzia tukio hilo kwa tabu, Tambwe alisema kuwa haelewi chanzo cha tatizo hilo kwani alitoka nyumbani kwake akiwa salama na alipofika uwanjani alianza mazoezi kama kawaida, lakini ghafla alisikia maumivu makali ya tumbo na baadaye hali kuwa mbaya zaidi.

“Sielewi chanzo cha tumbo hili maana nikiangalia kama ni chakula jana (juzi) nilikula cha kawaida, lakini namwachia daktari ambaye amenipa dawa nafikiri nitapata nafuu,” alisema Tambwe.

Tambwe aliyeibuka mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Kagame, lililofanyika nchini Sudan hivi karibuni baada ya kufunga mabao sita, alisema hiyo inaweza kuwa ni hali ya hewa na anaamini atakuwa fiti kabla ya Jumamosi.

“Yawezekana haya ni mabadiliko ya hali ya hewa na sina mashaka na hili naamini mpaka Jumamosi nitakuwa fiti kuikabili Ruvu Shooting ambayo imeonekana kuwa nzuri kwani inashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi,” alisema Tambwe.

No comments:

Post a Comment