Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

WENGER ASALIMU AMRI, SASA AKUBALI KUTUMIA PAUNI MIL 65 KUNUSURU KIBARUA CHAKE

 
LONDON, England

KATIKA kile ambacho kinaonekana ni kutaka kunusuru kibarua chake, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ametangaza kuvunja kibubu na kukwangua pauni milioni 65 ili aweze kurejea tena kwenye soko la usajili.

Wenger ambaye kwa sasa amekalia kuti kavu, baada ya timu yake kuanza msimu huu vibaya kwa kuambulia kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Aston Villa alitangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia jana huku akisema kuwa bado anatafuta ufumbuzi mwingine na kwamba atazitumia fedha hizo kwa ajili ya kusaka nyota wengine kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu ya England.
Kwa sasa Gunners imeshatangaza dau la pauni milioni 12 ikimsaka kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Yohan Cabaye dau ambalo limekataliwa na  Newcastle ambayo inataka dau hilo liongezeke zaidi.

Hata hivyo kwa mujibu wa  Starsport klabu hiyo iliyokumbwa na mgogoro inawawinda nyota wengine watatu ambao huenda wakaigharimu pauni hizo milioni 65.

Wanaotajwa kuwa mawindo ya timu hiyo ni nyota wawili wa timu ya  Swansea, Michu na  Ashley Williams pamoja na nyota wa Manchester City, Micah Richards, ambaye mwenyewe binafsi anataka kujiunga na  Gunners.

Awali kabla ya kutangaza nyota hao, Arsenal  iliwahi kujaribu kurusha karata yake kuwashawishi nyota wengine kama  Luis Suarez, Wayne Rooney na  Gonzalo Higuain,lakini ikashindwa na badala yake kocha  Wenger akajikuta akikaliwa kooni na mashabiki kwa kushindwa kutumia fedha msimu huu.


Mfaransa huyo tayari ameshaomba radhi kwa mashabiki kufuatia kipigo hicho cha mabao 3-1  kutoka kwa  Aston Villa  ikiwa nyumbani na usiku wa kuamkia jana aliwatumia ujumbe wa barua pepe uliosomeka: "Tunataka mashabiki wetu wawe na furaha. Unaposhindwa kufikia mafanikio hayo ni lazima ujihisi mnyonge na mwenyekuchanganyikiwa. Watu wanadhani hatutaki kutumia fedha ila tunataka kuzitumia."

No comments:

Post a Comment