Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

PELLEGRINI AKUNWA NA USHINDI WA KWANZA NA MOYES AMTABIRIA MAKUBWA VAN PERSIE

 
LONDON,  England

KOCHA Manuel Pellegrin ameelezea kufurahishwa alivyoanza kibarua chake  Manchester City,  baada ya kuibuka na ushindi wa mabao  4-0 dhidi ya Newcastle katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Ligi Kuu ya England.

Hata hivyo pamoja na kuanza vizuri, kocha huyo mpya Man City alikataa kusema kuwa kikosi chake tayari kimeshakuwa mmoja wa timu pinzani katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu licha kuonesha kiwango kizuri.

Katika mechi hiyo iliyopigwa usiku wa kuamkia jana alikuwa ni David Silva ambaye alipachika bao la kuongoza dakika ya sita kabla ya Sergio Aguero, Yaya Toure na  Samir Nasri kuzifumania nyavu za  Toon ambayo nyota wake,  Steven Taylor alitolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu kabla ya timu hizo kwenda mapumziko.
Akizungumzia ushindi huo, Pellegrini alisema: "Huu ni mwanzo mzuri na kwa kuwa tumeshinda ugenini tunataka kuendelea kucheza vizuri.

"Sisi hatukuwa na lengo moja ama mawili bali tulidhamiria kufanya vizuri  zaidi, lakini kwa sasa hatuwezi kujilinganisha na Manchester United ama Chelsea ambazo nazo zimeshinda kwani bado ni mapema,”alisema kocha huyo.

Akizungumzia kuhusu mchezaji wake, Vicent Kompany ambaye aliumia dakika za mwisho za mchezo huo, majeraha ambayo yanasadikika kuwa  ya nyama za misuli ya paja Pellegrini, alisema kuwa nyota huyo huenda akakaa bechi kwa muda wa wiki moja ama mbili.

@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 
Moyes amtabiria makubwa Van Persie

LONDON, England

KOCHA wa Manchester United, David Moyes amemtabiria makubwa mshambuliaji wake, Robin Van Persie akisema kuwa kuna mambo mengi mazuri  yanakuja kutoka kwa nyota huyo.

Msimu wa 2011-12, Van Persie aliifungia Arsenal mabao 30 kwenye michuano ya Ligi ya England  na kisha msimu uliopita akaifungia Manchester United mabao 25 yaliyomfanya apewe kiatu cha dhahabu kinachotolewa kwa mfungaji bora wa ligi kila mwaka.


Alipohojiwa kama Van Persie anaweza kuvuka mafanikio aliyoyapata katika msimu wake wa kwanza akiwa Manchester United,  Moyes alisema: "Nina matumaini anaweza kufanya hivyo.
"Mabao aliyofunga dhidi ya  Swansea ni zaidi ya mabao ambayo yamewahi kufungwa na wafungaji bora  na kwa jinsi unavyoweza kuona kuna vitu tofauti amevifanya,”alisema kocha huyo.

.

No comments:

Post a Comment