Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

BENNI McCARTHY ANAMKUBALI MOURINHO

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

KLABU ya Porto ya Ureno ilipata mafanikio makubwa ikiwa chini ya Kocha Mkuu wa sasa wa Chelsea, Jose Mourihno huku baadhi ya wachezaji waliotoa mchango kwenye timu hiyo akiwa ni McCarthy ambaye alishaitumikia Timu ya Taifa ya Afrika Kusini maarufu kama Bafana Bafana.

Katika mahojiano na gazeti moja la The Guardian la Afrika Kusini, McCarthy anasema kuwa Jose Mourihno ni kocha mzuri, kwani katika kipindi cha misimu miwili kuanzia 2002 hadi 2004 aliyokaa na Porto aliiwezesha kupata mafanikio ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kutwaa taji la UEFA na taji la Mabara.

“Kucheza soka kumenifanya niwe katika hali nzuri na kuweza kuinua maisha mazuri pamoja na familia yangu, hivyo kwa mafanikio hayo mchezo huo nauheshimu na kuupenda.

“Nimefurahia mno maisha yangu ya soka ambayo yalitoa kutoka katika timu za mtaani na hatimaye baadaye kuiwezesha klabu yangu ya Porto ambayo nilikuwa naichezea kutwaa taji la UEFA na kuichezea timu yangu ya Taifa ya Afrika Kusini katika michuano ya Kombe la Dunia, hivyo hayo ni mafanikio makubwa,” anasema McCarthy.

McCarthy akitokea katika mazingira ya kimasikini katika timu za mchangani hadi kuchezea katika ligi kuu kama za Hispania, Ureno, England na kutwaa Mataji akiwa na Ajax ya Uholanzi na Porto ya Ureno.

Pamoja na kuichezea klabu ya Porto ya Ureno kwa mafanikio makubwa, pia timu ya Taifa ya Afrika Kusini wanafahamu mchango wake, baada ya kudumu nayo kwa muda wa miaka miaka 16 kuanzia 1997 hadi 2012, akicheza mechi 79 na kufunga mabao 32.

McCarty ambaye alistaafu soka akiwa na umri wa miaka 35 ana mambo mengi ya kujivunia lakini akiwa na ameshapachika mabao 161 baada ya kushuka dimbani mara 387 zikiwemo mechi za timu ya taifa.

Katika michuano ya fainali za Mataifa huru Afrika ya mwaka 1998 iliyofanyika nchini Burkina Faso, McCarthy pamoja na mshambuliaji wa Misri, Hassan Hassan waliibuka vinara kwa upachikaji wa mabao na McCarthy kutangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo. 

Katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1998 zilizofanyika nchini Ufaransa Bafana Bafana mchezo wa kwanza ilifungwa Ufaransa ambao walikuwa Mabingwa wa taji hilo mabao 3-0, mchezo wa pili dhidi ya Denmark katika dakika ya 13 walikuwa wamefungwa bao moja, lakini katika dakika ya 52 McCarthy akisawazisha kuipa matumaini ya kusonga mbele.

Lakini hata hivyo katika mchezo wa tatu matumaini hayo yaliyeyuka baada kutoka sare na Saudia Arabia na hivyo kutolewa baada ya kushika nafasi ya tatu.

McCarthy akiwa na Bafana Bafana katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002 zilizofanyika Korea na Japan, historia ya kutofanya vizuri ilijirudia, kwani katika mchezo wa kwanza ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Paraguay, ilishinda mechi ya pili bao 1-0 dhidi ya Slovenian, lakini ilijikuta ikiaga michuano hiyo na kuwa mshindi wa tatu baada ya kufungwa na Hispania mabao 3-2.

Kihistoria mshambuliaji huyo mahiri ambaye alizaliwa Desemba 11, 1977 katika Mji wa Cape Town, Afrika Kusini pamoja na kuichezea Porto ya Ureno, pia katika vipindi tofauti vya nyuma amezichezea Blackburn Rovers, West Ham United za England, Celta Vigo ya Hispania, Ajax ya Uholanzi, Orlando Piretes na Seven Stars za Afrika Kusini. 

No comments:

Post a Comment