Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

UCHAGUZI WA TFF MOTO, WAMBURA NA MANJI WAJIENGUA

KATIBU Mkuu wa zamani wa Chama cha soka Tanzania (FAT) hivi sasa Shirikisho la soka Tanzania (TFF),  Michael Wambura ameshindwa kujitosa katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi yoyote ndani ya taasisi hiyo  baada ya kushindwa kutokea kwenye zoezi la uchukuaji na urejesaji wa fomu lililofungwa jana jioni.

Awali kwenye kinyan’ganyiro cha kwanza cha uchaguzi huo, ambao mchakato wake ulivurugika, Wambura alijitosa kugombea nafasi ya Makamu wa Urais nafasi ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Nassib Ramadhani na Wallace Karia.

Pia katika uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board), unaotarajiwa kufanyika Oktoba 18 mwaka huu, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji naye ameshindwa kujitosa katika kinyan’ganyiro cha uchaguzi huo, kama alivyofanya awali katika mchakato wa kwanza.

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura alilieleza DIMBA kwamba jumla ya wadau wa soka 58 wamejitokeza kuomba ridhaa ya kuwania nafasi mbalimali kwenye uchaguzi huo.

Baadhi ya walioomba ridhaa hiyo Athuman Nyamlani, Jamal Malinzi, Omari Nkwarulo na Richard Rukambura ambao wameomba kuwania nafasi ya Urais huku nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Madega, Nasib Ramadhani na Wallace Karia.

Baadhi ya wagombea kwenye nafasi za ujumbe ni pamoja na Jumbe Magati, Mugisha Galibona, Samwel Nyalla, Ally Mtumwa,
Ahmed Mgoyi, Ayoub Nyenzi, Cyprian Kuyava, Eliud Mvela,  Geoffrey Nyange ‘Kaburu’, Davis Mosha, Juma Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Abdulkadir, Shaffih Dauda na Wilfred Kidao.
  
Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni Hamad Yahya (Mwenyekiti) na Said Muhamad (Makamu Mwenyekiti).Walioomba nafasi za ujumbe ni Kazimoto Muzo, Michael Kaijage, Omari Mwindadi, Salum Rupia na Silas Magunguma.


No comments:

Post a Comment