Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, August 20, 2013

FEDHA ZINAAMUA MAISHA YA WACHEZAJI

KWA hakika mpira wa miguu ni biashara kubwa kwa sasa duniani.
Matajiri wengi kwa sasa wamewekeza katika mchezo huo unaopendwa na wengi na hiyo inachangia kuufanya upendwe zaidi.

Wachezaji wa mchezo huo wanahusudu zaidi fedha kuliko kitu kingine na aghalabu mchezaji kukaa katika klabu moja ilhali kuna klabu ambayo inaweza kumlipa zaidi ya hapo alipo.
Roman Abramovich ni mmoja kati ya matajiri wakubwa wanaomiliki klabu ya Chelsea ya nchini England.
 Abramovich si rafiki wa kweli hata kidogo, amewahi kuwatimua makocha nane waliokuwa wakiifundisha timu hiyo.

Makocha wapo kwa ajili ya kutimuliwa, lakini hiyo hutokea pale mafanikio yanapokosekana. Kwa wengine huwa raha mustarehe na hufurahia maisha. Sir Alex Ferguson ni mfano mzuri kwa Manchester United, kwani ameweza kudumu katika klabu hiyo kwa miaka 27 kuanzia mwaka 1986 hadi 2013 hadi alipoamua kujiweka pembeni.

Wakati mwingine fedha ina jeuri na inaweza kuamua kila kitu, ingawa kuwa nazo wakati mwingine si njia ya kupata kile unachohitaji katika maisha.
Angalia jeuri ya pesa, tajiri Roman Abramovich alivyowatimua kazi Claudio Raineri, Jose Mourinho, Avram Grant, Lusi Felipe Scolari, Carlo Ancelotti, Andre Villas-Boas, Roberto Di Matteo.

Hivi ndio fedha inavyofanya kazi katika mpira wa miguu, yote hii ni katika kusaka mataji.
Kazi sasa imerudi kwa Jose Mourinho ‘The Special One’ ambaye aliwahi kutimuliwa na tajiri huyo, amerejea tena Stamford Bridge kukinoa kikosi hicho.
Haya ndio maisha yalivyo katika mpira wa miguu, yamejaa kila aina ya vituko lakini ndivyo yanabadilisha maisha ya watu na kuyaboresha.

Hii ni biashara kubwa kwa kuwekeza na inalipa.
Wapo wachezaji waliotoka katika familia za kimaskini barani Afrika, waliopata utajiri kupuitia mchezo huu, tena ni watu wa kuheshimika si Afrika pekee, bali ni duniani kwa ujumla.

Wana fedha za kutosha, tena siku hizi wanawajali na wenzao kwa kuwekeza katika vituo vya michezo ‘Academy’.
Kwa kweli wanakumbuka kule walipotoka, ni jambo zuri na linapaswa kuigwa na wachezaji wengine hasa wa Tanzania.

Lakini ni safari ndefu sana kwa wachezaji wetu wa Tanzania wanahitaji kupitia ili kufikia huko na kutimiza ndoto za namna hii, kwa sasa ni wachezaji wawili pekee ambao angalau unaweza kusema wanaweza kutimiza ndoto hizo, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaocheza soka la kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Lakini wakati fulani niliwahi kusikia kuhusiana na Renatus Njohole Foundation, bado mpango huu haujaimarika, lakini nadhani ni njia nzuri ya kusaidia wengine.

Kwa kweli fedha zinaamua maisha ya wachezaji, Samuel Etoo ‘Fills’ aliondoka Inter Milan na kujiunga na  Anzhi Makhachkala ya nchini Russia kwa kuangalia fedha, wakati mwingine mchezaji huangalia fedha kwanza na mengine yatafuatia baadaye.


Fedha ndio huamua maisha ya mchezaji, lakini baadaye ya mshiko ni mataji, ndio maana Abramovich aliwatimua makocha kwa kuwa alikuwa akihitaji kitu kingine baada ya fedha.

No comments:

Post a Comment