WAKATI
imeripotiwa kuwa mshambuliaji hatari wa timu ya APR, Jean Cloud Irangi huenda
akawemo katika kikosi cha Yanga msimu ujao, mchezaji huyo amewataka mabingwa
hao wa Ligi Kuu Bara wasikurupuke katika kufanya usajili wake.
Akizungumza
na Lenzi ya michezo kwa njia ya simu, Iranzi alisema atakuwa tayari kuchezea timu yoyote
iwe Yanga, Simba au hata Azam FC, kama tu itaweza kufikia makubaliano na klabu
yake ya APR, ambayo amedumu nayo kwa miaka mitano sasa.
Alisema
kinachotakiwa ni viongozi wa timu zitakazohitaji saini yake, kuketi na uongozi
wa APR na kufikia makubaliano kwa vile anatambua umuhimu wa kuondoka kwenye
klabu hiyo akiwa na ridhaa ya viongozi wake.
“Unajua
huku ni nyumbani inanipasa niondoke nikiwa na ridhaa ya ‘wazazi’ (APR),”
alisema.
Hivi
karibuni klabu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti vimeeleza kuelekeza macho
yao katika klabu ya APR kwa ajili ya kumng’oa mshambuliaji huyo chipukizi wa
timu hiyo.
Mshambuliaji
huyo ambaye kwa sasa ametimiza miaka 20, aliwahi kuichezea timu ya watoto ya
Kiyovu kabla ya kujiunga na timu ya wakubwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2008, kisha
kujiunga na APR mwaka uliofuata, mahali ambapo anaendelea kucheza hadi sasa.
No comments:
Post a Comment