KIUNGO
mshambuliaji wa Simba, Amri Kiemba, amesema yupo tayari kupokea ofa ya timu
yoyote ikiwamo Yanga kama tu itamfuata na ofa nono, ili kuipata huduma yake
msimu ujao.
Kiungo
huyo, Kiemba, aliyewahi kuichezea Yanga, ambaye kwa sasa anamaliza mkataba wake
katika klabu ya Simba, alisema hawezi kuchagua timu ya kuchezea na anachosubiri
ni kupata ofa nono hilo ndilo analohitaji.
Kiemba
amesema kwamba, kwanza ataanza kwa kuwafuata viongozi wa klabu yake ya
Simba kujadili juu ya mkataba mpya, kama watasuasua kumpatia dau analohitaji
basi ataangalia ofa nyingine zitakazoletwa mezani kwake.
"Bado
sijazungumza na Simba juu ya mkataba mpya. Msimu utakapomalizika, nitawafuata
viongozi na kutaka kutambua hatima yangu, nitatazama kama watakuwa
wameniandalia ofa nzuri," alisema.
"Ninachokiangalia
mimi ni maslahi, kama Simba hawatakuwa na ofa nzuri na kisha klabu yoyote ikaja
na ofa yake nzuri, nitakuwa tayari kujiunga nao. Milango kwangu ipo wazi,
kikubwa ni maslahi tu."
Kiungo
huyo wa kimataifa wa Tanzania, anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na
Jumamosi hii anatarajia kuwamo kwenye kikosi cha Simba kitakachomenyana na
Yanga katika mchezo wa funga dimba wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Katika
mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo msimu huu, uliomalizika kwa sare ya
bao 1-1, Kiemba ndiye aliyeifungia bao la kuongoza Simba kabla ya Yanga
kusawazisha kwa mkwaju wa penalti kupitia Said Bahanuzi.
No comments:
Post a Comment