KIUNGO wa Manchester
United, Paul Scholes amethibithisha kuwa atatundika daluga mwisho wa msimu huu.
Scholes (38), aliwahi
kutundika daluga mwisho wa msimu wa 2010-11, lakini baada ya kufanya kazi ya
ukocha kidogo alirudi uwanjani, Januari 2012, baada ya kuona kwamba alichukua
uamuzi wa mapema mno kustaafu soka Old Trafford.
Majeruhi yamemfanya
acheze kidogo msimu huu, huku akishindwa kucheza mechi yoyote ya Ligi Kuu
England, mwaka 2013.
Katika mahojiano na
mchezaji mwenzake wa zamani, Gary Neville anayefanya kazi ya utangazaji kwenye
kituo cha Sky Sports, Scholes alisema kwamba huu ni wakati muafaka kwake
kutundika daluga.
Alipoulizwa kama atakuwa
kwenye kikosi cha David Moyes msimu uajo: Scholes alijibu: “Hapana. Naamini huu
ni wakati wa kustaafu. Haukua msimu ambao ningetaka kustaafu. Miezi minne
iliyopita imekuwa migumu kwangu. Najua akilini mwangu kuwa nimemaliza kila
kitu.”
Hii inamaana Scholes
atastaafu wakati mmoja na Sir Alex Ferguson, na kiungo huyo hakusita kumfagilia
Ferguson, huku akiamini kuwa Moyes atafanya vizuri Old Trafford.
No comments:
Post a Comment