KLABU ya Tout Puissant
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo inajivunia
washambuliaji wawili wa Kitanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu
itamenyana na Liga Maculmana ya Msumbiji kuwania tiketi ya kucheza hatua ya
makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika. Hiyo inafuatia upangwaji wa droo ya hatua
ya 16 Bora ya michuano hiyo, inayodhaminiwa na Orange mjini Cairo, Misri leo.
Katika droo hiyo, AS FAR Rabat ya Morocco iliyoitoa Azam FC katika Kombe la
Shirikisho imepangwa kukutana na wapinzani wao, FUS Rabat. Katibu Mkuu wa CAF,
Hicham El Amrani aliongoza droo hiyo kwa pamoja na wawakilishi wa baadhi ya
klabu zinazoshiriki michuano hiyo. Klabu nane zilizotolewa katika Ligi ya
Mabingwa, St George, CA Bizerte, TP Mazembe, Enugu Rangers, JSM Bejaia, FUS
Rabat, Stade Malien na Entente Setif zimeingia kwenye mbio za kuwania kurithi
taji la AC Leopards ya Kongo, mabingwa wa Kombe la Shirikisho na mechi za kwanza
zitachezwa kati ya Mei 17, 18 na 19 mwaka huu wakati marudiano yatakuwa kati ya
Mei 31 , Juni 1 na 2. Mazembe ambao ni mabingwa mara nne Afrika, walitolewa na
Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika Raundi ya Tatu ya Ligi ya Mabingwa kwa
jumla ya mabao 3-2, wakifungwa 3-1 Afrika Kusini na kushinda 1-0
nyumbani. DROO KAMILI YA 16 BORA
KOMBE LA SHIRIKISHO: Stade Malien (Mali) vs Lydia
(Burundi) Enugu Rangers ( Nigeria) vs C.S.S (Tunisia) FUS Rabat ( Morocco)
vs ASFAR (Morocco) CAB (Tunisia) vs Ismailia (Misri) E.S Setif ( Algeria)
vs US Bitam (Gabon) JSM Bejaia ( Algeria) vs E.S.S (Tunisia) TP Mazembe
(DRC) vs Liga Maculmana (Msumbiji) St George (Ethiopia) vs ENPPI (Misri)
NMB YAPELEKA ELIMU YA FEDHA KWA MAELFU YA VIJANA
-
Benki ya NMB imesisitiza umuhimu wa kupeleka elimu ya fedha kwa umma
sambamba na kupanua huduma rasmi za kifedha, ikisema ujumuishaji wa kifedha
unahita...
Leadership and Teamwork, Defined by the Serengeti
-
If you want a masterclass in leadership, style, and pure majesty, you don't
look to a boardroom you look to the plains of the Serengeti.
Watching an e...
Uchumi : Rais Samia Aipa BOT Dira Mpya
-
Na Janeth Raphael MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameielekeza
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuongeza uwezo wa kuc...
WASIRA AWATOLEA UVIVU WALIOANZA MBIO ZA URAIS
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Stephen
Wasira, Leo Machi 27, 2026, Mjini Bunda Mkoa wa Mara alipokuwa akiweka
jiwe la ms...
Post a Comment