MACHIFU WATUMA UJUMBE WA AMANI
Machifu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamewahimiza Watanzania kuendelea kudumisha maridhiano, mshikamano na amani kama msingi wa ustawi wa taifa, kupitia Tamasha la Asili la Bulabo 2026 linaloendelea katika Viwanja vya Ngomeni-Kisesa, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.Wamesema amani na umoja ni nguzo muhimu katika kulinda urithi wa kitamaduni na kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Mwenyekiti wa Tamasha la Bulabo, Jackson Kadutu, akizungumza kwa niaba ya machifu hao, amewataka vijana kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na badala yake kutumia majukwaa ya utamaduni kujifunza, kuendeleza na kuhifadhi mila na desturi za Kitanzania.
Machifu hao pia wameeleza kuwa maadili mema ya Kiafrika yanapaswa kurithishwa kwa kizazi cha sasa ili kuhakikisha tunu za taifa zinaendelea kuheshimiwa na kulindwa.
Tamasha la Bulabo 2026 lenye kaulimbiu isemayo, “Maridhiano kwa Njia ya Amani Ndiyo Jadi Yetu, Linda Maadili ya Mtanzania”, lilianza Juni 7 na linatarajiwa kuhitimishwa Juni 14, 2026, likiwakutanisha machifu kutoka Tanzania, nchi za Afrika Mashariki na Afrika Kusini kwa lengo la kuenzi utamaduni, kuimarisha mshikamano na kukuza maadili ya Kiafrika.

Post a Comment