Mrisho Ngassa akipokea jezi kutoka kwa Katibu wa Yanga Lawrance Mwalusako |
Karibu kijana, Ngasaa akisalimiana na Mwalusako |
Kama kawaida yake aachi kubusa jezui ya Yanga |
Ngasa akivaa jezi yake |
MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga Mrisho Khalfan ‘Ngassa’ ameibuka na kusema kuwa amerejea nyumbani
katika timu anayoipenda katika maisha yake yote.
Kauli hiyo ya Ngassa aliitoa katika utambulisho wake wa
kujiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza katika utambulisho huo, Ngassa alisema anamshukuru
Mungu sambamba na viongozi wa klabu hiyo waliorejesha katika timu anayoipenda.
“Ninamshukuru Mungu viongizi wangu kwa kufanya jitihada za
kunirudisha katika klabu hii ambayo nina mapenzi nayo ya dhati,”alisema.
Alifafanua kuwa klabu ya Simba haina shukrani kwa kila
alichokifanya ndani ya klabu hiyo ndio sababu ya kuikacha.
“Nimeisaidia sana Simba lakini hawana shukurani, kila sana
lawama wakati nilikuwa bado sijasaini Yanga yalikuwa maneno tu,”alisema
Alisema kuwa ujio wake ndani ya Yanga anaimani utasaidia
kukuza kipaji chake alichonacho.
“Nashukuru mashabiki wangu waliokuwa na mimi toka Azam, Simba
hivyo naomba tuungane kuijenga Yanga,”alisema.
Alipoulizwa mkataba wake ndani ya Simba, Ngassa alisema kuwa
hana mkataba na klabu hiyo kwa kuwa waliingia mkenge kumsainisha wakati mtu
akiwa mchezaji wa mkopo huwezi kumsainisha.
“Sijasaini Simba ile gari aina ya verosa ilikuwa ni ushawishi
wa kunitoa Azam na kuja kwa mkopo kwao hivyo huwezi kumsainisha mtu ambaye ni
mchezaji wa mkopo,”alisema
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa kamati ya usajili Abdallah
Binkleb alisema walianza mazungumzo an Ngassa miezi sita nyuma bila ya
kuvunjika moyo.
“Ngassa amedhihirisha
yeye ni mchezaji wa uhakika na mwenye nidhamu maana mbali ya kutangaza kuhamia
Yanga lakini alicheza mechi zake ndani ya Simba kwa kiwango cha hali ya
juu,”alisema.
Ngassa alitua Simba SC kwa mkopo Agosti mwaka jana akitokea
Azam FC ya Dar es Salaam pia, ambayo nayo iliamua kumtoa kundini baada ya kukerwa
na ‘Uyanga wake’.
Hata hivyo, Simba SC ilifanikiwa kuipiku Yanga SC kwa kuuziwa
mchezaji huyo kwa Sh. Milioni 25 kwa mkopo. Lakini alipotua Simba SC, ikaelezwa
aliongeza mkataba wa mwaka mmoja na kupewa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni
12 fedha taslimu na Milioni 18, thamani ya gari aina ya Verosa.
Lakini Ngassa mwenyewe alisema alipewa Milioni hizo 30 ili
akubali kushuka Msimbazi na si kusaini mkataba mpya.
Ngassa alisajiliwa Azam Mei 21, mwaka 2010, kwa dola za
Kimarekani 40,000, zaidi ya Sh. Milioni 60 kutoka Yanga SC, huku yeye mwenyewe
akipewa dola 30,000, zaidi ya Sh. Milioni 45.
No comments:
Post a Comment