Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 19, 2013

NAY WA MITEGO NA DIAMOND PLATINUMZ WAFUNIKA KWENYE UZINDUZI WA VIDEO '' MUZIKI GANI'' DAR LIVE!

Nay wa Miego akiburudisha umati wa watu waliojitokeza kwa wingi Darlive!
DAR Live usiku wa kuamkia leo ilitikisika baada ya mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia onyesho la pamoja kati ya wanamuziki wawili nyota wa kizazi kipya, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' na Ney wa Mitego ambao walikuwa wakizindua video ya wimbo wao wa 'Muziki Gani'.

Wanamuziki hao kwa pamoja walitoa burudani ya nguvu ambayo ilizikonga nyoyo za mashabiki waliofurika katika ukumbi huo wa maraha uliopo Mbagala Zakhem, jijini Dar.
Diamond Platnumz akiwapa hi mashabiki.
Ney wa Mitego akiwarusha wapenzi wa burudani.
Nyomi iliyoitikia shoo hiyo. Kitu na box full kimyaaa!!!Nipe na mimi Hi jamani Diamond...Wasafiiii..Jukwaa likitetemekaHii balaa jukwaani jamani...Nay na Diamond wakitupia maneno ya kwenye Video Muziki gani jukwaani live...Jamani nani zaidi??? Hip Hop na mbana pua!!!

Diamond na Ney wakiwapagawisha mashabiki.
Ney wa Mitego akisema na wapenzi wake.
Diamond Platnumz akionyesha umahiri wake stejini.

Diamond akifanya makamuzi sambamba na kundi lake.
ilikuwa show moja matata sana hip hop v bongo flava

No comments:

Post a Comment