|
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Almas Kasongo |
KAMATI
ya Ufundi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),
kimetangaza kuanza kwa Ligi ya vijana walio chini ya umri wa miaka 15,
itakayoanza Julai 29 mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Ufundi wa DRFA, Joseph Kanakamfumu, alisema jana baada ya kikao cha
kamati hiyo, kilichokutana jana (Jumapili) kwenye Ukumbi wa Harbours Club
Kurasini kuwa ligi hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho katika
kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam unaibua vipaji kwa faida ya mkoa na
Taifa.
Ligi
hiyo itakuwa na faida kubwa kutokana na kuenda sawa na umri unaotumika na
mashindano ya vijana ya Copa Coca Cola, ambayo mwaka huu yameanza kwa
kushirikisha umri wa miaka 15.
Pia
alisema ligi ya wanawake itaanza Agosti mwaka huu huku akiomba wadhamini
nao kujitokeza kusaidia ligi hizo.
Wakati
huo huo fomu kwa ajili ya kozi ya waamuzi na ile ya mpira wa miguu kwa
ngazi ya cheti cha pili (Inter-Mediate) na zinapatikana kwenye
ofisi za vyama vya mpira vya wilaya vya IDFA, KIFA na TEFA.
|
No comments:
Post a Comment