Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 6, 2013

JUVENTUS YATWAA UBINGWA ITALY SERIE A!!!


MABINGWA WATETEZI wa Italy, Juventus, jana wametwaa tena Ubingwa wa Italy kwa kuifunga Palermo Bao 1-0 huu ukiwa Ubingwa wao wa 29. 

Penati ya Dakika 59 ya Arturo Vidal ndio iliwapa ushindi na Ubingwa Juventus huku wakiwa na Mechi 4 mkononi kwa vile wako Pointi 14 mbele ya Timu ya Pili Napoli ambayo haiwezi kuzifikia.
Hii ni mara ya kwanza katika Miaka 10 kwa Juve kutwaa Mataji mara mbili mfululizo ukiondoa yale Mataji ya Misimu ya Miaka ya 2005 na 2006 ambayo walinyang’anywa baada ya kupatikana na hatia ya kupanga Matokeo Mechi.
Ukiondoa hayo Mataji mawili, Juve sasa rasmi wana Mataji 29 yakiwa Mataji 11 kupita Timu nyingine yeyote huko Italy.
Penati hiyo ya Juve ilipatikana baada ya Massimo Donati kumsukuma Mirko Vucinic lakini Juve walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Paul Pogba, kupewa Kadi Nyekundu kwa kumtemea mate Beki wa Palermo Salvatore Aronica.


Mara baada ya Juve kutwaa Ubingwa, Klabu ya AC Milan ilituma ujumbe uliosema: "CONGRATULAZIONI ALLA JUVENTUS FC - CAMPIONE D'ITALIA." ukimaanisha: “HONGERA JUVENTUS KWA KUWA BINGWA WA ITALY!”
Title winner: Vidal celebrates his goal with arms outstretched
Mabingwa tena:Vidalakishangilia
Spectacle: A giant banner of the Juventus crest is unfurled prior to kick-off, as thousands of fans wave black and white flags
Mabango na bendera ulifika wakati wake mashabiki wakaamasisha kutwaa ubingwa huo
Juventus supporters display a giant flag at their Italian Serie A soccer match against Palermo
Juve kidume!!!
Hero: Juventus coach Antonio Conte soaks up the acclaim of the crowd
Kocha wa Juventus Antonio Conte akiwapungia mashabiki baada ya mechi kuisha
Italy's best: Juventus fans create a colourful display during the game
Mashabiki wa juve wakinyoosha bendera juu
MSIMAMO WA JUU ULIVYO KWA SASA.Serie A - The top six

No comments:

Post a Comment