Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 6, 2013

CHELSEA YAILAZA MAN UNITED 1-0, CHELSEA YAPANDA NAFASI YA TATU


Ligi kuu England iliyoendela jana jumapili kati ya United na Chelsea Bao la Dakika ya 87 la Juan Mata likiguswa na Beki Manchester United Phil Jones na kumbabaisha Kipa Anders Lindergaard na kutinga wavuni na kuipa Chelsea ushindi wa Bao 1-0 Uwanjani Old Trafford hii leo katika Mechi ya BPL, Barclays Premier League, na kuwafanya wachupe hadi nafasi ya 3.

Hata hivyo, mara baada ya Chelsea kufungua Bao hilo Man United walimlalamikia Refa Howard Webb kwani muvu ya Bao hilo ilianza wakati Man United wanashambulia na Wayne Rooney kuchezewa rafu na Ramirez na kuupoteza Mpira uliokwenda kuzaa Goli.
Sasa Chelsea, waliocheza Mechi moja pungufu ukilinganisha na Arsenal, wako Pointi 1 mbele ya Arsenal walio nafasi ya 4 na Pointi 3 mbele ya Tottenham.

Mara baada ya Goli hilo, Mchezaji wa Man United Rafael alionyeshwa Kadi Nyekundu baada ya kuvaana na David Luiz kitendo ambacho kilizaa rabsha kidogo huku Wachezaji wa Man United wakilalamika Luiz alikuwa amehadaa ili Rafael apewe Kadi Nyekundu.Robin van Persie akijaribu kumtoka David Luiz huku Phil Jones naye akinyemelea karibuRobin Van Persie kigo awafunge Chelsea kwa kichwaBosi wa Manchester Unite Sir Alex Ferguson akicheki mtanangeKocha wa Muda wa Chelsea Rafa Benitez naye jicho kwa jicho akiangalia vijana wake jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford.Veteran wa United Giggs akiruka juu kutwaa mpira dhidi ya Cesar Azpilicueta wa Chelsea.Mchezaji Rafael Da Silva akitolewa nje kwa kadi nyekundu na refa Howard Webb baada ya kucheza ndivyo sivyo kwa David LuisWanajuana hawa...Veteran Ryan Giggs kwenye patashika na frank LampardRooney akiingia kuchukua nafasi ya AndersonBeki Phil Jones akimchanganya kipa kwa kugusa mpira bahati mbaya na mpira huo kuishilia nyavuni katika dakika za mwishoni.Juan Mata akishangilia mara tu baada ya kuipatia Blues bao la dakaka za majeruhi dakika ya 87 na kufanya 1-0 dhidi ya United ambao ndiyo mabingwa wa msimu huu wa 2012/2013Rooney, RVP, veteran Giggs Hoiiii....VIKOSI:
Man Utd: Lindegaard, Da Silva, Evans, Vidic, Evra, Jones, Anderson (Rooney 69), Cleverley (Buttner 68), Valencia (Hernandez 90), Van Persie, Giggs.
Subs Not Used: De Gea, Ferdinand, Scholes, Kagawa.
Sent Off: Da Silva (89).
Booked: Vidic, Jones.
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Ivanovic, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Oscar, Mata (Ake 90), Moses (Torres 76), Ba.
Subs Not Used: Turnbull, Ferreira, Cahill, Terry, Benayoun.
Booked: Luiz.
Goals: Jones og 87.
Att: 75,500
Ref: Howard Webb

No comments:

Post a Comment