ARSENAL YAIFUNGA QUEENS PARK RANGERS 1-0, YATINGA TOP 4
Leo Washika bunduki wa
London Arsenal wakicheza Ugenini kwa QPR Loftus Road Uwanja uliojengwa mwaka
1904, Bao la Theo Walcott la sekunde 20 tu baada ya kipenga cha Refa Jon Moss
kupulizwa limewapa ushindi mtamu Arsenal na kupanda hadi nafasi ya tatu wakiwa
na alama 67 chini ya Manchester City wenye Pointi 72 ambao pia leo wametoshana
nguvu ya bila kufungana na timu ya Swansea City iliyopanda Daraja msimu huu
unaomalizika hivi karibuni.
Ushindi huu pia unampa
nafasi tena baada ya kutoka suruhu wiki iliyopita walipocheza na United. Ngoma
inabaki kwa Chelsea ambao pia bado wanamichezo mingi na huku wakiwa na alama 65
sawa na Spurs wakipitwa na alama 2 tu, hivyo Arsenal bado wapo kwenye hali tete
kwani timu hizo zikicheza na kupata ushindi zitamgoa Arsenal nafasi hiyo ya
tatu.
Arsenal sasa wamebakisha
michezo 2 tu kufunga msimu huu na kujihakikishia nafasi ya kuwemo kwenye 4 bora
ili kushiriki kombe la UEFA Champions.
Gunners Pia wanabakiwa na mchezo nyumbani kati ya Wigan utakao chezwa tarehe 14 mwezi wa tano siku ya Jumanne saa 9:45 mchana na kisha kuelekea
Newcastle kucheza mchezo wa
kumaliza msimu ambao utachezwa kwa muda mmoja na timu zote 20 za ligi kuu
England, Mchezo utakao chezwa tarehe 19 mwezi huu wa tano tarehe 19 siku ya
Jumapili saa 12:00 jioni.
Theo Walcott naJi-Sung Park wakichuana vikali leo hii
Arsene Wenger akiangalia vijana wake wakiminyana na timu
kibonde inayoshuka daraja QPR
Tal Ben Haim na Aaron Ramsey wakigombania mpira
Loic Remyakimkingia kifua Aaron Ramsey wa Arsenal
Hapa hupiti:Theo Walcott na Stephane Mbia wakichuana
Tulia ...huko......
Andros Townsend na Nacho Monreal wakikimbizana
Pongezi kwako Theoooo...
VIKOSI:
QPR: Green, Ben Haim, Onuoha, Hill, Traore (Da Silva 90), Townsend, Jenas, Mbia (Derry 46), Remy, Park (Taarabt 79), Zamora.
Subs Not Used: Murphy, Mackie, Granero, Bothroyd. Booked: Derry, Jenas.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Ramsey, Arteta, Rosicky (Vermaelen 90), Walcott, Cazorla (Wilshere 89), Podolski (Oxlade-Chamberlain 85).
Subs Not Used: Mannone, Coquelin, Jenkinson, Gervinho.
Booked: Monreal.
Goal: Walcott 1.
Attendance: 18,178
Referee: Jon Moss
MATOKEO YA MECHI ZA LEO BPL
Jumamosi 4 Mei
[Saa 11:00 Jioni]
Fulham 2 v Reading 4
Norwich 1 v Aston Villa 2
Swansea 0 v Man City 0
Tottenham 1 v Southampton 0
West Brom 2 v Wigan 3
West Ham 0 v Newcastle 0
[Saa 1:30Usiku]
QPR 0 v Arsenal 1

Post a Comment