Mchezaji Burhan Ally wa Polisi Zazibar(blue) akirudisha mpira kwa upande wa Twalipo kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya Muungano |
Wachezaji wa Twlipo wakimsikiliza kocha wakati wa mapumziko |
Wachezaji wa Polisi Zanzibar wkisikiliza kocha wao Haji Uzia Vuai (aliyevaa kofia) wakati wa mapumziko |
Wachezaji wakitapeana fair play baada ya mchezo |
TIMU ya mpira wa kikapu ya Polisi Zanzibar leo imeshika nafasi ya tatu
kwenye mashindano ya Muungano yaliyokuwa yanafanyika kwenye uwanja wa ndani wa
Taifa kwa kuifunga Twalipo ya Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulichezwa majira ya asubuhi jana
ulishuhudia Polisi Zanzibar ikiongoza kwa seti na kufanya kushika nafasi
ya tatu.
Kwenye seti ya kwanza Polisi walongoza kwa seti 25 kwa 22, seti ya pili
25 kwa 22 na seti ya tatu iliongoza tena kwa seti 31 kwa 29 za Twalipo Dar es
Salaam.
Akizungumza jijini, kocha wa timu ya Polisi , Haji Uzia Vuai alisema
anashukuru kwa nafasi waliyoshika kwani mashindano yalikuwa magumu kutokana na
timu kuajiandaa vema ili wao hawakuwa na maandalizi kutokana na kubanwa na
kazi.
“Sisi hatukufanya maandalizi yoyote ila tulikuja kushiriki kwani
Muungano ni wetu sote hivyo nafasi tuliyoshika si haba kwa inabidi tukajiandae
vema ili mwakani tufanye vema zaidi”, alisema Vuai.
Naye nahodha wa Twalipo, Talib Mohamed alisema wamepoteza mchezo
kutokana kuzidiwa ujanja na wapinzani wao na kutumia vema nafasi walizozipata
hivyo ni changamoto kwao kujiandae vema kwa mashindano yajayo.
No comments:
Post a Comment