KLABU ya Bayern Munich ya Ujerumani imetoa taarifa kupinga kwamba wamefikia makubaliano ya uhamisho na mshambuliaji wa Borussia DortmundRobert Lewandowski. Wakala wa mshambuliaji wa kimataifa wa Poland, Maik Barthel jana alidai kuwa mteja wake huyo anataka kuondoka Dortmund katika kipindi cha majira kiangazi na kuongeza kuwa wameshafikia makubaliano binafsi na klabu nyingine na kuzua uvumi kwamba atahamia Bayern. Hata hivyo Bayern wamebainisha kuwa hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa kwamba tayari wamemsajili Lewandowski.Lewandowski mwenye umri wa miaka 24 ana mkataba na Dortmund unaomalizika mwaka 2014 lakini ameshatoa msimamo wake kuwa hana mpango wa kuongeza mkataba mwingine na klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment