Mechi za BPL, Barclays Premier League, zitachezwa Jumamosi kwa kuanza na Man City na West Ham Uwanjani Etihad.
Lakini mkazo utakuwa huko Emirates ambapo Arsenal itabidi waweke Gwaride la Heshima kwa Man United kabla Mechi kuanza hapo Jumapili ikiwa ni kuwapa heshima inayostahili Man United kwa kutwaa Ubingwa wa England walipowafunga Aston Villa Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford Jumatatu iliyopita.
Kitu ambacho kitawachoma baadhi ya Mashabiki wa Arsenal ni kumuona aliekuwa Nahodha wao, Robin van Persie, akiingia Uwanjani na Timu yake Man United na kuwekewa Gwaride la Ubingwa ambalo hakulipata Arsenal kwa Miaka 8 aliyodumu hapo hadi ahamie Man United mwanzoni mwa Msimu huu.
Akiwa na Man United, Van Persie ndie anaongoza Listi ya Mfungaji Bora wa BPL akiwa a Goli 24, 3 ambazo alifunga Jumatatu iliyopita Man United ilipowachapa Villa 3-0 na kutwaa Ubingwa.
Mchezaji wa zamani wa West Bromwich Albion wa mwaka 1972 na Manchester miaka ya 1981 Bryan Robson(kulia) akiwa na Bosi Sir Alex Ferguson wa Manchester United leo kwenye mazoezi wakiangalia wachezaji wakifanya mazoezi kabla ya Man United kukutana na Arsenal Jumapili hii
Robin van Persie na wenzake wakifanya mazoezi leo hii
Wachezaji wa United, Rio Ferdinand na Tom Cleverley kulia wakifanya mazoezi leo hii
Jumamosi 27 Aprili
[Saa 8:45 Mchana]
Man City v West Ham
[Saa 11 Jioni]
Chelsea v Swansea
Everton v Fulham
Southampton v West Brom
Stoke v Norwich
Wigan Tottenham
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Newcastle v Liverpool
Jumapili 28 Aprili
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Reading v QPR
[Saa 12 Jioni]
Arsenal v Man United
Jumatatu 29 Aprili
[Saa 4 Usiku]
Aston Villa v Sunderland
No comments:
Post a Comment