Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, March 14, 2013

GENNARO GATUSO KUTUNDIKA DARUGA RASMI MAJIRA YA JOTO


Kiungo nyota wa zamani wa kimataifa wa Italia na klabu ya AC Milan, Gennaro Gattuso amesema anatarajia kustaafu rasmi kucheza soka katika kipindi cha majira ya kiangazi ili aweze kuhamishia nguvu zake kwenye ukocha.

Gattuso mwenye umri wa miaka 35 ambaye kwasasa anacheza katika klabu ya FC Sion ya Switzerland amedai anadhani wakati wa kutundika daruga umefika baada ya kucheza kwa kipindi cha miaka 18.

Nguli huyo amesema mara baada ya kuacha kucheza soka anataka kujitolea kwa nguvu zake zote katika kazi yake mpya ya ukocha ili aweze kupata mafanikio kama ilivyokuwa wakati akicheza soka.

Nyota huyo aliendelea kudai kuwa amepata uzoefu wa kutosha wakati akiwa mchezaji chini ya makocha Marcello Lippi na Carlo Ancelotti kwani walikuwa walimu wazuri kwake wakati akiwa Milan.

FC Sion ambayo kwasasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu nchini Switzerland maarufu kama Swiss Super League wanatarajia kusafiri kwenda Geneve Jumapili kupambana na timu ya Young Boys.

No comments:

Post a Comment