Wednesday, March 6, 2013
ANOUMA ASHINDWA RUFAA CAS, ISSA HAYATOU HANA MPINZANI KWENYE UCHAGUZI
Rais wa shirikisho la soka nchini Ivory Coast ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka duniani FIFA Jacques Anouma ameshindwa rufaa yake ya akipinga sheria iliyomzuia kushirikia uchaguzi wa Rais wa shirikisho la soka barani Afrika CAF akiwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo katika uchaguzi ambao umepangwa kufanyika wiki ijayo.
Mahakama ya kimataifa ya michezo (CAS) hapo jana imesema kuwa imekubaliana na mabadilioko yaliyofanywa na CAF mwezi septemba mwaka jana ambayo yanataka wagombea wa nafasi ya Urais watoke katika kamati ya utendaji ya shirikisho hilo.
Taarifa iliyotolewa na CAS hapo jana imesema kuwa mabadiliko yaliyofanywa na CAF mwezi septemba mwaka jana ni halali kutumika katika uchaguzi uchaguzi huo na kwamba kwa mujibu wa mabadiliko hayo ni kwamba Anouma amekosa sifa hiyo muhimu ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa shirikisho hilo la soka barani Afrika.
Rais wa sasa wa CAF Issa Hayatou atakuwa akiingia katika uchaguzi bila mpinzani akiwania nafasi ya Rais kwa kipindi kingine cha miaka minne ya uongozi wa shirikisho hilo la soka barani Afrika ambao utafanyika jijini Marrakech nchini Morocco jumapili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment