Hans Pope ambaye amewasilisha barua yake ya kujiuzulu leo kwa mwenyekiti wa klabu hiyo,Ismail Aden Rage amedai kuwa ameamua kuachia ngazi kutokana na mwenendo mmbaya wa timu hiyo ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita ilijikuta ikitolewa kwa aibu katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika ilipokubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Recreative de Libolo ya Angola na kufanya kutolewa kwa
jumla ya mabao 5-0 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kwenye uwanja wa taifa wiki mbili zilizopita.
Klabu hiyo ya
mtaa wa Msimbazi licha ya kuchemsha kwenye michuano ya klabu bingwa pia
imeonekana kusuasua katika Ligi Kuu ya Tanzania bara ambayo Yanga inashika
nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 39 wakati Simba ipo
nafasi ya tatu kitendo ambacho kinaiweka pabaya kutetea ubingwa
wake.
Sababu kubwa inayoonekana kusababisha mwenendo mbaya ndani ya kikosi hicho ni pamoja na usajili mbovu ambao ulikua ukisimamiwa na Mwenyekiti huyo hali iliyosababisha kusajili wachezaji kwa mamilioni ya pesa na baadae kuwaacha.
Miongoni mwa wachezaji aliowasajili na wengine kuacha ni pamoja na Kamonbil Keita,Patrick Ochieng,kipa Dhaira,Emmanuel Okwi.
Hans Pope aliyekuwa jembe la usajili la Simba, amesema ameamua kuachia nafasi yake hiyo kutokana na mambo yanavyokwenda.
Uongozi wa Simba kupitia kwa Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Geofrey Nyange 'Kaburu' alidhibitisha kujiuzulu kwa Hans Pope.
"Hans Pope amejiuzulu na amewasilisha barua leo akimuandikia mwenyekiti ikieleza nia yake hiyo ya kujiuzulu hata hivyo mwenyekiti kwa sasa hayupo nchini yupo India kwa matibabu."
Kujizulu kwake ni pigo kwa Simba ambayo imekuwa ikienda kwa mwendo wa kuyumba huku ikiwa haina nafasi ya kutetea ubingwa.
Tangu kuingia kwake madarakani kiongozi huo ambae alikua akitumia mamilioni ya pesa katika kusajili amejikuta akiingia katika mgogoro na uongozi wa timu hiyo pamoja na wanachama wao wakidai imefanya usajili usio na tija kwa klabu hiyo.
Hans Pope aliyekuwa msaada mkubwa ndani ya klabu hiyo katika usajili , amesema ameamua kuachia nafasi yake hiyo kutokana na mambo yanavyokwenda pamoja na kumaliza majukumu aliyokabidhiwa na uongozi.
Alisema kufuatia kumaliza muda wake wa kuitumikia klabu hiyo ameona ni vyema akatoa nafasi kwa wengine kushika nyadhifa hiyo kwa lengo la kuleta mabadiliko ndani ya klabu hiyo.
"Sijashinikizwa na mtu katika
maamuzi yangu,nimeamua mwenyewe baada ya kuona muda wangu wa kuitumikia
Simba umemalizika kwani nataka kuwaachia na wengine,naamini kabisa majukumu niliyopewa nimeyakamilisha kikubwa tuendelee kushikamana katika kuiendeleza
timu hii"alisema
Hans pope.
Hans pope.
Aliongeza"Kama
timu inafanya vibaya ni heri kuwaachia wengine wajaribu kwani si vizuri lawama
ni bora,kifanye kitu kwa mafanikio na
wanachama waridhike na mwenendo wa timu kwa hali hii sioni kama nastahili
kuendelea kuingoza Simba".Makamu mwenyekiti wa Simba, Kaburu alisema
uongozi umepokea barua ya kiongozi huyo na kwamba wataijadili na kuitolea
maamuzi pale kamati ya utendaji ya klabu hiyo itakapokutana siku yoyote kuanzia
sasa. Mtawala alisema Hans Pope alikua Mwenyekiti wa kuteuliwa hivyo
wanafanya mawasiliano na Mwenyekiti wao aliyepo India kwa matibabu na
watakaporuhusiwa kuzungumza lolote ndio watatoa kauli kama
uongozi.
Simba ambayo imeondolewa katika hatua ya awali ya michuano ya kimataifa ya klabu bingwa Afrika pia imejikuta ikiweka ubingwa wake rehani baada ya kufanya vibaya katika baadhi ya mechi zake za ligi. Timu hiyo itashuka dimbani tena jumapili kuikabili Coastal union ya Tanga kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment