BAADA ya kocha wa Azam Stewart Hall kufungiwa michezo mitatu na faini uongozi wa timu ya
Azam umeliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kuomba kocha wao
msaidizi Kali Ongala aruhusiwe kukaa
benchi la timu hiyo
Kali ambaye atambuliki kama kocha kwa kuwa hana vyeti vinavyo
mtambulisha amesomea ukocha hawezi kutambuliwa bila TAFCA kuthibitisha.
Kamati ya ligi kuu ilitangaza kumfungia
kocha Stewart mechi tatu na faini ya
Sh 500,000 kwa kosa la kuvua bukta uwanjani wakati wa mchezo wao dhidi ya Kagera
Sugar.
Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa
Nassor alisema kuwa baada kufungiwa kocha wao wameiandikia barua TFF, kuomba wamruhusu Ongala kukaa benchi mpaka
uchunguzi wa vyeti vyake utakapokamilika.''Ongala alifungiwa lakini
tulishapeleka vyeti vyake muda mrefu lakini mpaka sasa wamekaa kimya hivyo
tumewaandikia barua ya kumruhusu kocha huo msaidizi mpaka pale
watakapojiridhisha na uchunguzi wao'' alisema Nassoro.
Katika hatua nyingine, Nassor
alisema kuwa timu yao inatarajia
kuondoka nchini Jumamosi Asubuhi kwenda Sudan kusini kwa ajili ya kucheza mchezo
wao wa marudioano dhidi ya El Nasri Juba.Alisema wanatarajia kupata upinzani
mkubwa ugenini kwa kuwa nia yao na ya
kwao wote ni kuakikisha wanasonga mbele katika michuano hiyo.
Alisema timu itaondoka ikiwa na
wachezaji 20 na viongozi saba tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Jumapili
No comments:
Post a Comment