Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 27, 2012

SIMBA YANG'ANG'ANIA KILELENI, YALAMBA ICE CREAM ZA AZAM TAIFA

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akimpongeza mshambuliaji mwenzake Felex Sunzu alifunga bao la kwanza

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akienda kufunga bao huku beki wa Azam Ibrahim Shikanda akimzuia kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akienda kufunga bao huku beki wa Azam Agrey Morris akijaribu kuokoa kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa

Mshambuliaji wa chipukizi wa Simba Ramadhan Singano wa Simba akiwatoka beki wa Azam Sahm Nuhu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Taifa

Wachezaji wa Simba wakitoka uwanjani kwa furaha ya ushindi wa mabao 3-1

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao kwenye mchezo  wa ligi kuu Tanzania uliochezwa uwanja wa  Taifa leo





TIMU ya Simba imefunga Azam FC mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Ushindi huo, unaifanya Simba izidi kukaa kileleni mwa ligi kwa kufikisha pointi 22, baada ya kucheza mechi 10, wakati Azam FC inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 18, baada ya kucheza mechi tisa. Nafasi ya pili inashikiliwa na abaada ya kufikisha pointi 20 leo kwa kuifunga JKT Oljoro

Mabao ya Simba yametiwa kimiani na Emanuel Okwi mawili na Felix Mumba Sunzu Jr. moja na mabao ya Azam yamefungwa na John Bocco ‘Adebayor’.

Hadi mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao 2-1, Azam wakitangulia kufunga dakika ya nne, kupitia kwa Adebayor ambaye alimtoka beki Mkenya Paschal Ochieng.Sunzu aliisawazishia Simba bao dakika mbili baadae, akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi ya Mrisho Khalfan Ngassa kutoka wingi ya kulia.Okwi aliifungia Simba bao la pili dakika ya 40, baada ya kutokea kizaazaa langoni mwa Azam kufuatia mpira uliopigwa langoni na Mwinyi Kazimoto.    

Kipindi cha pili Simba kilianza kwa Simba kushambulia na iliwachukua dakika tano tu kuhitimisha karamu yao ya mabao 3-1, baada ya Okwi kuwainua tena vitini mashabiki wa Simba, akifumua shuti la mbali, baada ya kuwatoka mabeki wa Azam.
Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Paschal Ochieng, Shomary Kapombe, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix Sunzu, Mrisho Ngassa na Emmanuel Okwi.
Azam FC; Mwadini Ali, Ibrahim Shikanda, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad na Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Jabir Aziz, Himid Mao, John Bocco ‘Adebayor’, Kipre Herman na Salum Abubakar.


Matokeo mengine ya Mechi za leo ni kati ya African Lyon na Kagera Sugar ambao wametoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam

Huko Arusha uwanja wa  Sheikh Aman Karume Yanga wameifunga JKT Oljoro bao 1-0 lililifungwa na Mbuyi Twite dk 57

Ruvu Shooting wameifunga Polisi Morogoro mabao 2-1 kwenye Uwanja wa  Mabatini, Mlandizi.

Ligi itaendelea kesho kwa michezo kati ya JKT Ruvu na Coastal Union Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Toto Africans dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

No comments:

Post a Comment