Meneja
wa Chelsea, Guus Hiddink, alitumia Dakika 20 na kutaka Kikosi chake
kijiangalie wenyewe kwenye Kioo na kujiponda wenyewe.
Hiddink, mwenye Miaka 69 na aliewahi kuwa Kocha wa Netherlands kwa mara kadhaa, aliteuliwa Wiki iliyopita kumbadili Jose Mourinho alietimuliwa Alhamisi iliyopita na kupewa wadhifa huu hadi mwishoni mwa Msimu huu.
Hivi sasa Chelsea, ambao ni Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 15 baada ya Mechi 17 za Ligi wakiwa Pointi 3 tu juu ya zile Timu 3 za mkiani ambazo mwishoni mwa Msimu huporomoka Daraja.
Hiddink amesema Chelsea inaweza, kimahesabu, kumaliza ndani ya 4 Bora Msimu huu ili icheze UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao lakini ni kazi ngumu.
Amesema: “Hii Ligi ni ngumu. Kila Timu inaweza kumuua mwenzake.”
Hii ni mara ya pili kwa Hiddink kutua Chelsea na mara ya kwanza ilikuwa Msimu wa 2008/09 alipotimuliwa Luiz Felipe Scolari na yeye kushika wadhifa wa Umeneja kwa Miezi Mitatu ya mwisho akiwasaidia Chelsea kutwaa FA CUP, kufika Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI na kumaliza Nafasi ya 3 kwenye Ligi wakiwa Pointi 7 nyuma ya Mabingwa Manchester United.
Kuhusu kuwepo kwake Stamford Bridge, Hiddink alieleza: “Sipaswi kuwa hapa baada ya nusu Msimu kwisha. Ina maana mambo hayaendi vizuri. Lakini nina furaha kurudi. Miaka michache nyuma ilikuwa hali kama hii.”
Aliongeza: “Ubingwa hapa si rahisi. Ukitwaa Ubingwa unabweteka na kisha unaamshwa. Si rahisi kusema niko hapa na kila tatizo limekwisha.”
Kuhusu Kikosi chake, Hiddink alisema: “Nimeongea nao na tumezungumza yaliyopita..kwa nini niko hapa..kwa nini tuko chini. Lakini pia niliwaambia kwenye Soka mambo mengi hutokea na nimemtaka kila Mtu ajitazame mwenyewe kwenye Kioo, si kwa Sekunde moja tu bali muda mrefu.”
Kuhusu Mashabiki wao, Hiddink aliasa: “Natumai Mashabiki wataisapoti Timu kama walivyofanya kidogo Gemu iliyopita. Lakini Timu lazima ije juu. Ninachojua kuhusu Chelsea ni kuwa Mashabiki huwa nyuma ya Timu lakini Timu lazima ionyeshe uwezo wake kwanza.”

No comments:
Post a Comment