Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, May 24, 2016

YANGA MIKONONI MWA TP MAZEMBE CAF



SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF) leo limepanga droo ya hatua ya makundi ya michuano yake ambapo Yanga inayoshiriki kombe la Shirikisho Afrika imepangwa kundi moja na TP Mazembe ya DR Congo.
Mazembe imejizolea umaarufu nchini hasa baada ya kuinyanyasa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011.
Lakini pia Watanzania wamekuwa wakiifuatilia kutokana na kusajili wachezaji wawili wa kitanzania Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anacheza Ugiriki na Thomas Ulimwengu ambaye bado yupo Mazembe.
Kwa mujibu wa droo ya CAF jana mchana, Yanga imepangwa kundi B na Mazembe, Mo Bejaia ya Algeria na Modeama ya Ghana.
Yanga ilifika hatua hiyo baada ya kuiondosha Sagrada Esperanca ya Angola kwa jumla ya mabao 2-1 katika hatua ya 16 ya michuano hiyo ya Shirikisho baada ya kuondolewa na Al Ahly ya Misri kwenye Ligi ya Mabingwa. mechi za makundi zinatarajiwa kuanza kuchezwa mwezi ujao.
Kwa upande wa kundi B zipo timu za Kawkab Athletic, Fath Union Sports za Morocco, Etoile du Sahel ya Tunisi na Ahly Tripoli ya Libya.
Katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Zesco ya Zambia imepangwa kundi moja na Al Ahly ya Misri, Asec Mimosas ya Ivory Coast na Wac ya Morocco. Kundi B lina timu za Enyima ya Nigeria, Zamalek ya Misri, Es Setif ya Algeria na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment