Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 24, 2015

ARSENE WENGER ATAKA MENEJA WA MAN UNITED APEWE MUDA ZAIDI, WAKALA JORGE MENDES ASEMA MAN UNITED HAIMUHITAJI JOSE MOURINHO

Van Gaal
Arsene Wenger amewataka Watu kuacha kuzungumzia habari za Meneja wa Manchester United Louis van Gaal kuhusu hatima yake na kusema kufanya hivyo ni utovu wa nidhamu.
Baada ya kutoshinda katika Mechi na kufungwa Mechi 3 mfululizo za mwisho ambapo mojawapo iliwabwaga nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI na kuwatupa UEFA EUROPA LIGI kumekuwepo na shinikizo kubwa la kutimuliwa Mdachi huyo kutoka Man United.
Hata hivyo, Van Gaal bado yupo Man United na Leo kuendelea na Mazoezi kama kawaida na baadae ataongea na Wanahabari kwenye Mahojiano ya kawaida kabla ya Mechi yao ya Jumamosi ya Ligi Kuu England na Stoke City.
Shinikizo hilo la kutimuliwa kwa Van Gaal limekuja Siku chache baada ya Chelsea kumtimua Jose Mourinho ambae sasa anatajwa sana kumrithi Van Gaal huko Man United.
Lakini hii Leo Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, ambae pia ndie Wakala wa Wachezaji kadhaa Mastaa wakiwemo David De Gea na Cristiano Ronaldo, amekanusha kuwepo na chochote kati yao na Man United kuhusu Mourinho kujiunga nao.
Nae Wenger amesema: “Sitaki kuingia kwenye uvumi. Mimi ninamuheshimu sana Van Gaal na nadhani hiki kinachoendelea ni kukosa heshima. Huyu Mtu amefanya kazi Zaidi ya Miaka 30 kwenye Soka na utumishi uliotukuka. Ni lazima anahitaji kupewa muda zaidi!”