Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, May 14, 2017

SERENGETI BOYS KUTUPA KARATA YAKE KESHO
KESHO timu ya Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 ‘Serengeti boys’ wanatarajiwa kutupa karata yao ya kwanza katika fainali za 12 za mashindano ya Afrika zinazofanyika nchini Gabon kuanzia leo.

Serengeti boys ambayo tayari wapo Gabon tangu Mei 7 zitakuwa fainali zitakuwa fainali zao za kwanza  huku watanzania wakiweka matumaini makubwa kwao pengine wanaweza kututoa kimasomaso.

Kikosi hiki cha Serengeti boys kimeandaliwa kuleta ushindani kwani kimecheza michezo saba ya kirafiki ya kimataifa, kati hizo  imeshinda michezo mitano, sare mmoja na kufungwa mmoja.

Tanzania itakuwa na wachezaji 21 ambao wamepitishwa na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambazo zitakuwa fainali za 12 toka kuanzishwa kwa michuano hiyo ambapo tamati yake itakuwa Mei 28.
Timu shiriki zimegawanywa katika makundi mawili; kundi A lina timu za wenyeji Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana na kundi B lina timu za Tanzania, Mali, Niger na Angola
Kundi A ndilo linafungua dimba leo ambapo wenyeji Gabon wanacheza na Guinea ikifuatiwa na Cameroun ambaye ataoneshana ubabe na Ghana mjini Port Gentil.
Kundi B, litaanza kutupa karata zao kesho ambapo Serengeti boys itafungua dimba na bingwa mtetezi Mali , kwenye Uwanja wa Franceville, Libreville na kufuatiwa na mchezo wa Angola dhidi ya Niger.
Mchezo huo utachezwa saa 9:00 za Gabon ambapo ni sawa na saa 12:00 za Tanzania.
Mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Niger Mei 18 saa 9:00 za Gabon sawa na saa 12:00 za Tanzania
Mchezo wa mwisho kwenye makundi itacheza na Angola, Mei 21 saa 2:00 mbili usiku sawa na 5:00 usiku za Tanzania.
Timu zitakazofuzu nusu fainali zitakuwa zimefuzu kuwakilisha Afrika katika fainali za FIFA U-17 zitakazofanyika nchini India kuanzia Oktoba 06-28, 2017.

Katika kuhakikisha Serengeti boys inafanya vizuri wadau mbalimbali wamejitokeza kuichangia timu hiyo ambayo ni mara ya kwanza kushiriki baada ya kufuzu na kuondolewa baada ya kumchezesha Nurdin Bakari ambaye alikuwa amezidi umri.
Serengeti boys ni timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo ilifuzu baada ya kutolewa kwa Congo Brazaville iliyomchezesha mchezaji aliyezidi umri.
Kocha wa Serengeti boys, Bakari Shime wamefanya maandalizi mazuri ambayo yanaifanya timu yake kuwa tayari kwa mashindano na lengo lao ni kubaki katika nne bora ili kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika India.
“Tuko tayari kwa mashindano.Mipango yetu inakwenda vizuri na tumecheza mechi saba ambazo zimeonesha maendeleo. Tunatarajia mashindano magumu lakini tutapambana ili kufikia malengo yetu, “alisema Shime.
“Ari ya wachezaji iko juu.Sasatunaweza kusema kuwa tuko tayari kwa mashindano na tunawaomba Watanzania kutuunga mkono.”alisema Shime
Serengeti boys ilipiga kambi Morocco kwa takribani siku 21, ambapo ilicheza na Gabon katika mechi mbili za kirafiki, ambapo ilishinda 2-1 katika kila mchezo.
Kambi ya mwisho ilikuwa Yaounde, katika mji mkuu wa Cameroon, ambako timu ilipumzika kwa siku nane. Serengeti iliwashtua wenyeji kwa kuifunga 1-0 katika mchezo wa kwanza kabla ya kupoteza kwa idadi hiyo ya bao katika mchezo wa marudiano.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu kabla Serengeti boys kuondoka Morocco kuweka kambi aliiandalia chakula cha jioni huku akiwaasa wachezaji hao kupigana kufa na kupona kwani watanzania wanapenda kusikia wanafanya vizuri.
Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akiongoza harambee ya kuichangia timu hiyo hafla iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) alisema wana imani na Serengeti boys kuwa inakwenda kufanya vizuri na kuichangia shilingi milioni tano.
Wadau mbalimbali na vyama vingine vya michezo vimetoa salamu nyingi kuitakia heri Serengeti boys ambayo Jumatatu itakuwa Uwanjani kumenyana na bingwa mtetezi, Mali.
Katika kuonesha kila kitu kipo tayari Shirikisho la Soka barani Afrika limepitisha orodha ya wachezaji 21 kwa kila timu ambazo zinashiriki fainali hizo.
Yafuatayo ni majina 21 ya wachezaji wa Serengeti boys waliopitishwa na nafasi watakazokuwa wanacheza na mwaka aliozaliwa .
Kikosi cha Serengeti boys kilichopitishwa ni makipa
Ramadhan Kabwili,  Samwel Edward, Kelvin Kayego:
Mabeki ni Enrick Vitalis, Dickson Job, Issa Makamba, Ally Msengi Nickson Kibabage
Viungo ni Kelvin Nashon, Shaaban Ada, Cyprian Benedictor, Saidi Mussa, Ally Ng’anzi
Washambuliaji:Yohana Mkomola, Muhsin Malima, Ibrahim Abdallah. Israel Mwenda, Kibwana Ally, Mohamed Rashid, Assad Juma ,Abdul Suleiman