SIMBA
imepata ushindi wa pili mfululizo kwenye Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara
baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye mchezo mkali
uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.
Kwenye mechi
iliyopita Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya hasimu wake Yanga kwa
bao lililofungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, ambae
pia alifunga bao la pekee la Simba kwenye mchezo wa leo
Kutokana na
matokeo hayo Simba imeendelea kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu
ya Soka ya Tanzania Bara ikiwa nyuma kwa pointi moja dhidi ya Mtibwa Sugar
inayoshika nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi Yanga wenye pointi 31.
Kwenye
mchezo wa jana Mtibwa Sugar walitangulia kubisha hodi kwenye lango la Simba
lakini shuti la mshambuliaji wake Ally Sharif, lakini akiwa peke yake na kipa
Ivo Mapunda wa Simba alipiga shuti lililopaa juu ya lango.
Dakika tatu
baadae Simba walijibu kwa kufanya shambulizi kali lakini mshambuliaji wake
Elias Maguli alishindwa kuunganisha mpira wa krosi wa Simon Sserunkuma.
Emmanuel
Okwi kwenye dakika ya 16 akiwa ndani ya
eneo la penalti alipiga shuti lililotoka nje kidogo ya lango la Mibwa na dakika
ya 21 Okwi tena alipokea pasi ya kiungo
Saidi ndemla lakini shuti lake halikulenga lango.
Dakika ya 24
Henry Joseph alikaribia kuifungia Mtibwa Sugar lakini kichwa alichopiga
akiunganisha krosi ya Mussa Mgosi kilitoka nje la lango la Simba.
Mchezo
ulilazimika kusimama dakika ya 36 baada ya Ame Ally kugongana vichwa na kiungo
Abdi Banda wa Simba.
Mtibwa Sugar
walifanya mashambulizi mfululizo kwenye dakika ya 42 na 44 lakini wachezaji
wake Henry Joseph na Mussa Mgosi hawakuwa makini kutumia nafasi walizopata.
Okwi
aliyeisumbua sana ngome ya Mtibwa Sugar
alikaribia kufunga bao la kuongoza lakini shuti alilopiga akiwa katikati ya
mabeki lilitoka nje kidogo ya lango.
Mgosi,kwenye
dakika ya 47 alikosa bao la wazi baada ya kupokea pasi ya Henry Joseph, lakini
badala ya kufunga alijikuta akiunawa mpira huo hali iliyolazimu mwamuzi
Abdallah Kambuzi kutoka Shinyanga kumuonyesha kadi ya njano.
Simba
ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Simon Sserunkuma na kumuingiza Ramadhani Singano
kwenye dakika ya 55 na kwenye dakika ya 58 Juuko Murshid alikosa bao akishindwa
kutumia pasi nzuri ya Okwi.
Mtibwa Sugar
walifanya mabadiliko kwa kumtoa Ame Ali na kumuingiza Mohamedi Mkopi kwenye
dakika ya 65, mabadiliko ambayo
hayakuisaidia sana timu hiyo.
Akiwa
amebaki peke yake na kipa Said Mohamedi, Elias Maguli alipiga shuti lililopaa
juu ya lango baada ya pasi nzuri ya Okwi kwenye dakika ya 69.
Mtibwa
walifanya mabadiliko kwenye dakika ya 75 na dakika ya 86 walifanya mabadiliko
mengine kwa kumtoa Mzamili Selembe na kumuingiza Ally Yusuph, lakini mchezo huo
ukionekana kumalizika kwa sare ya bila kufungana Emmanuel Okwi aliwainua
mashibiki wa Smba kwa kufunga bao kwenye dakika ya 90 kwa shuti kali akiwa nje
ya eneo la penalti.
No comments:
Post a Comment