Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Liverpool kuvunja benki kwa Keita



Naby Keita RB Leipzig
LONDON, England
LIVERPOOL wapo tayari kuvunja benki ili wampate kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita.
Wekundu hao wapo tayari kutoa pauni milioni 50 ili watengeneze kikosi kitakachofanya vyema zaidi msimu ujao, ikizingatiwa kwamba Jurgen Klopp amewawezesha kuingia kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya (UCL), baada ya kumaliza Ligi Kuu ya England (EPL) wakiwa wkenye nafasi ya nne.
Wakitoa pauni milioni 50 watakuwa wamevunja pia rekodi ya klabu hiyo, ambapo Leipzig wameamua kumbandika mchezaji huyo bei hiyo ili kuwavunja matumaini ‘wachumba tarajali’.
Liverpool wanasema hiyo si kitu, na wapo tayari kuitupa mbali rekodi ya pauni milioni 38 walizotumia kumsajili And Carroll. Klopp anajipanga kuingiza majina makubwa Anfield kiangazi hiki.
Mjerumani huyo anaamini kwamba Keita, raia wa Guinea, ndiye mtu sahihi kwenye eneo la kiungo, akiieleza Bodi ya Wakurugenzi Liverpool kwambandiye bora zaidi kwa Ulaya sasa.
Kuna uwezekano mkubwa kwa Liverpool  kuvunja rekodi ya matumizi yao yajumla ya fedha za usajili, kwani walitumia pauni milioni 150, lakini sasa ikielezwa wanapanga kutumia kwenye pauni milioni 200 ili kwenda kwata moja na Manchester United na Manchester City. Keita atataka mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment